Tangazo

May 23, 2014

KINANA SEPUKA


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa amebeba Jogoo aliyepewa zawadi na wakina mama wa tawi la UWT Puma,Katibu Mkuu alifungua shina la wakina mama wajasiriamali wanaojishughulisha na kilimo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akishiriki kuvuna viazi vitamu pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai kwenye shamba la mkulima Bernardo Razalo
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa ofisi za CCM kata ya Ighombwe ambapo aliwahimiza viongozi wa CCM kujenga ofisi zenye uwezo wa kutoa  msaada wa kijamii ikiwa pamoja na elimu za ujasiriamali .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Ighombwe na kuwataka kudumisha moyo wa mshikamano katika kuleta maendeleo ya pamoja.
Mbunge wa Singida Magharibi Mh.Mohamed Misanga akihutubia wakazi wa Sepuka na kuwaambia hatua za kimaendeleo zilipofikia .
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga ngoma pamoja na kikundi cha ngoma cha Ihgombwe wilayani Ikungi.
Wasanii wa kikundi cha ngoma wakicheza ngoma ya Peni wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la ofisi za CCM kata ya Ighombwe.
Ndivyo wasemavyo wananchi wa Sepuka.
Wasanii wa kwaya kutoka Sepuka wakiburudisha kabla ya kuanza kwa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Sepuka, Ikungi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Sepuka na kuwataka kuungana katika kushiriki kuleta maendeleo hasa yale yanayohusu jamii kama kujenga shule, maabara na zahanati.

No comments: