Tangazo

May 25, 2014

MKUTANO WA KINANA -SINGIDA MJINI

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Singida mjini kwenye mkutano wa hadhara wa CCM ambapo aliwaambia kuwa lengo kubwa la ziara zake ni kukagua utekelezaji wa  ilani ya uchaguzi wa CCM na kukagua uhai wa chama, pia alitoa wito kwa wana CCM kujisahihisha kwenye mapungufu.
 Naibu Waziri wa Maji Ndugu Amos Makala akihutubia wakazi wa Singida mjini nakuelezea miradi ya maji inavyoendelea kukamilika na muda si mrefu maji yatakuwa sio tatizo kwa wakazi wa mji huo.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi Charles Tzeba akihutubia wananchi wa Singida mjini na kuwambia tatizo la usafiri wa treni limepatiwa ufumbuzi wa kudumu kwani Reli ya kati inaboreshwa na tayari vichwa 40 vya treni vitaanza kazi ifikapo Januari hivyo gharama za usafiri wa treni kwa abiria na mizigo itashuka.
 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone akihutubia wananchi wa Singida mjini na kuwaambia utekelezaji wa ilani ya uchagui umefanikiwa kwa kiasi kikubwa ambapo wananchi wengi wa mkoa huo wamejiandikisha kupata Bima ya Afya lakini pia hospitali kubwa ya mkoa inayojengwa ikikamilika itakuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa 1000.
 Mbunge wa Singida mjini akihutubia wananchi wa Singida wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katik viwanja vya People's mjini hapa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisaidiana na Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini Mohamed Dewji kukabidhi mifuko 50 ya Simenti kwa Taasisi za kidini.Ambapo kila taasisi ilipata mifuko 50.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi bati pamoja na Mohamed Dewji na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Lameck Nchemba kwa taasisi zaidi ya 80.Mbunge wa Singida mjini ametoa mabati 50 kwa kila taasisi ya kidini na mifuko ya Simenti 50.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Naibu Waziri wa Fedha Ndugu Adam Malima mara baada ya kumaliza mkutano wa Singida wengine kwenye picha ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone  na Mkuu wa Wilaya ya Singida Mjini  Queen Mlozi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye Bajaj katikati ya mitaa ya Singida.
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba akiwa kwenye Bodaboda pamoja na Mbunge wa Singida mjini Mohamed Dewji wakiwa njiani kuelekea eneo la mkutano wa hadhara.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiingia kwenye viwanja vya mikutano kwa usafiri wa Bajaj. Bajaj inayofuata kwa nyuma amepanda Ktibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma maelezo kutoka kwenye bidhaa za wakina mama wajasiriamali walioleta bidhaa zao kwenye mkutano wa CCM viwanja vya people's.
 Ktibu Mkuu wa CCM akiingia uwanja wa mkutano.
Wabunge wa CCM Singida wakinyoosha mikono juu kusalimia wananchi.

No comments: