Rais Dkt
Jakaya Mrisho Kikwete akionesha jedwali la alama za ufuatiliaji wa
utendaji wa huduma za afya ya mzazi na mtoto wakati wa uzinduzi wa Mpango
Mkakati wa Kuongeza kasi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya
watoto katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julis Nyerere jijini
Dar es salaam leo. Pamoja naye ni naibu Waziri wa Afya Dkt Kebwe Sthephen
Kebwe.PICHA/IKULU
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Na Magreth Kinabo – Maelezo
Rais Jakaya Kikwete
amewataka Wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha kuwa
wanasimamia Mpango Mkakati ulioboreshwa wa Kuongeza
Kasi ya Kupunguza vifo vya Uzazi vya wakinamama na watoto hususan
wachanga ili kutimiza malengo ya millennia namba nne na tano ifikapo mwaka
2015.
Aidha Rais Kikwete aliagiza viongozi
wa mapango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) kuliingiza suala la afya katika mpango
huo.
Changamoto hiyo imetolewa leo na
Rais Kikwete kabla ya kuzindua mpango huo, ulioenda sambamba na
uzinduzi wa kadi ya ufuatiliaji(scorecard) ambayo itakuwa inaonesha
tathimini na ya maendeleo na mkakati huo kwa kila mkoa na wilaya.
Rais Kikwete aliwataka wakuu hao na
watendaji wao kutoa ripoti ya kadi ya ufuatiliaji kila baada ya miezi minne.
Kadi hiyo, ambayo itakuwa na taarifa ya maendeleao ya kupunguza vifo vya watoto
wachanga, chini ya miaka mitano na wakinawajawazito.
Uzinduzi huo, uliofanyika kwenye
ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam.
Alisema vifo vya uzazi vya
wakina mama vimepungua kutoka 578 kwa vizazi hai 100,000 mwaka 2005 na kufikia
vifo 454 kwa vizazi hai 100,000 kwa sasa, wakati lengo la milenia ni vifo 193
kwa vizazi hai 100,000.
“ Bado tuna safari ndefu
ninawataka wakuu wa mikoa na wilaya kuchulikia jambo hili kwa umakini na kulipa
kipaumbele kwani jukumu hili si la waganga wakuu wa mikoa au wilaya na
mimi nitakuwa ninafuatilia kwa kuwa jambo hili, lipo mikononi mwangu.
Ninataka kulifuatialia kabla sijamaliza kipindi cha uongozi wangu,”
alisema Rais Kikwete.
Aliongeza kuwa vifo
hivyo vya wakina mama na watoto hutokea lakini havifatiliwi ndio maana inakuwa
vigumu kubaini njia za kuvipunguza.
“ Baya zaidi wanakufa kwa sababu
zinazoweza kuzuilika, kadi ya ufuatiliaji ikifuatiliwa na wakuu wa mikoa
itasaidia kupunguza vifo,” alisisitiza.
Alisema ikiwa watoto
waliochini ya miaka mitano na wakinamama wajawazito watazingatia masuala ya
lishe bora kwa kipindi cha siku 1000 pia itasaidia kupunguza vifo hivyo.Huku
akisema vyakula hivyo vipo majumbani kinachohitajika ni elimu.
Aliwataka wakimama kuzingatia
uzazi wa mpango(nyota ya kijani ) ili kusaidia kupunguza tatizo hilo, pia
kushirikisha wanaume juu ya jambo hilo.
Rais Kikwete pia alisema asilimia 51
ya wakina wanaojifungua huhudumiwa na watalaamu wenye ujuzi, wakati malengo ya
milinea ni asilimia 80, hivyo bado kuna changamoto ya asilimia 29.
Kwa Upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Kebwe Stephen Kebwe, alisema
kwa kipindi cha mwaka huu wanampango wa kuajiri watalaamu hao 11,021.
Alisema Tanzania imefanikiwa
kutimiza lengo la milinea namba nne kabla ya wakati kwa kupunguza vifo vya
watoto chini ya miaka mitano kwa kiwango cha 54 kwa watoto wanaozaliwa 1000,
kutoka 165 kwa wataoto wanaozaliwa 1000 mwaka 1990. Alizitaja nchi nyingine
zilizofanikiwa ni Rwanda, Malawi,Ethiopia Rwanda na Malawi.
Naye mwakilishi wa wakuu hao, Dk.
Christine Ishengoma alisema uwajibikaji wa viongozi na watendaji ni
jambo la muhimu katika kutekeleza mpango huo, hivyo suala hilo linawezekana.
Kaimu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri
Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Dk. Deo Mtasiwa
alisema sheria ndogondogo zinatengenezwa ili kuwezesha mpango huo kufikia
lengo.
Dk. Mutasiwa alizitaka
halimashauri kutumia vyanzo vyake vya mapato ya ndani kwa asilimia 60 kuwekeza
katika masuala ya afya, elimu maji na barabara za vijijini.
Alisema hivi sasa wako katika
mchakato wa kupata kibali cha kuwaezesha watoa huduma wa afya wanaomba nafasi
za kazi kufanyia kazi maeneo wanayotoka.
No comments:
Post a Comment