Amina Ngaluma enzi za uhai wake. |
Aliyewahi kuwa mwanamuziki wa dansi wa bendi za African
Revolution 'Wana tam tam' na Double M, enzi hizo chini ya uongozi wa Muumin
Mwinjuma, Amina Ngalum A.K.A Japanese (pichani enzi za uhai wake) amefariki
dunia nchini Thailand, ambako alikuwa akifanya shughuli zake za kimuziki.
Akizungumza na mtandao huu, mtoaji wa habari hizi, aliyewahi
kuwa Mkurugenzi wake katika bendi ya Tam Tam, Asha Baraka, amesema kuwa Amina
amefariki dunia wakati akifanyiwa upasuaji.
''Imeelezwa kuwa Amina alianza kuugua ghafla, huku akilalamika
kuwa kichwa kinamuuna na tumbo, na ndipo alipokwenda hospitali kwa ajili ya
kupima na kuambiwa kuwa alikuwa na uvimbe kichwani na hivyo kutakiwa kufanyiwa
upasuaji,
Aidha ilielezwa kuwa uvimbe huo ulikuwa ukitoa damu na baada ya
kuanza kufanyiwa upasuaji hakuweza kuamka tena na ndipo umauti ulipomfika''.
alisema Asha Baraka.
Mpaka mauti yanamfika, Amina alikuwa mwanamuziki wa bendi ya
Jambo Survivors.
Msiba upo Kipunguni B, Machimbo jijini Dar es Salaam.
MUNGU AILAZE ROHO YA
MAREHEMU AMINA MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!
No comments:
Post a Comment