Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwa na Rais mpya
wa Malawi Prof. Arthur Peter Mutharika wakiwa katika picha ya pamoja baada ya
rais mpya wa Malawi kukabidhiwa madaraka jijini Brantyre kwenye hoteli
Sunbird. Baada ya kukutana viongozi hao walipata fursa ya kuzungumzia masuala
la kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili na kukubaliana kuendelea kuwa na
mahusiano mema kama nchi zinazoishi ndugu na jirani. Picha kwa Hisani ya Ikulu
ya Malawi
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DkT. Mohammed Gharib Bilal leo Jumatatu
Juni 02, 2014 ameshiriki katika sherehe za kukabidhi madaraka kwa Rais mpya wa
Malawi Profesa Arthur Peter Mutharika katika sherehe zilizofanyika kwenye
uwanja wa Kamuzu Banda jijini Blantyre. Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Rais
wa Botswana sambamba na wawakilishi wa nchi za Zimbabwe, Msumbiji, Afrika
Kusini na nyinginezo.
Akihutubia baada ya
kukabidhiwa sime ambayo ni ishara ya kuwa kiongozi wa watu wa Malawi, Rais
Mteule Mutharika alisisitiza kuwa, katika kipindi cha utawala wake atahakikisha
kuwa anaifanyia makubwa Malawi sambamba na uhakikisha kuwa anaifanya Malawi
itimize majukumu yake ya kimataifa kufuatia kutambua kuwa kujitenga kunaweza
kuifanya Malawi kutonufaika na fursa zilizopo duniani.
“Nchi hii ipo katika
dunia na siyo rahisi tena kuwa na fikra kwamba Malawi inaweza kubaki peke yake
kama kisiwa. Tunahitaji kuwa na wenzetu wa kusaidia maendeleo ya Malawi.
Tunawahitaji wahisani toka Kusini ama Mashariki, tunayahitaji mataifa tajiri na
mataifa yanayoendelea. Tutafanikiwa sana kama tutaendeleza urafiki kwa wote.
Tufanye hivi bila kujali kuwa sisi ni taifa kwani hali ya sasa inahitaji kila
mmoja wetu kushirikiana na mwenzake,” alisema.
Katika hotuba hiyo pia
amesisitiza kuwa kipindi chake cha utawala atajitahidi kukabiliana na rushwa na
kwamba hatakuwa na mchezo kwa wala rushwa katika kipindi akiwa madarakani. Pia
alisisitiza kuhusu umuhimu wa kuiunganisha Malawi kwa miundombinu bora ili
kuboresha maisha ya wananchi sambamba na kusogeza huduma za wananchi karibu.
Rais Mutharika
aliapishwa juzi baada ya kuwashinda washindani wake akiwemo Rais aliyemaliza
kipindi chake Joyce Banda ambaye hata hivyo hakuweza kutokea katika sherehe
hizi za kukabidhi madaraka.
Akizungumzia suala la kutohudhuria kwa Rais Banda,
Rais Mteule Mutharika alisema alitegemea Rais Banda kuwepo lakini hakufika na yeye anatambua kuwa wakati wa uchaguzi kulikuwa na tofauti baina yao lakini kwa
sasa uchaguzi umeisha na amesahau yaliyopita ili kuanza ukurasa mpya wa
kuijenga Malawi. Katika shughuli hiyo pia Rais wa zamani wa Malawi Kamuzu Banda
alihudhuria.
Makamu wa Rais Dkt.
Bilal na msafara wake walitarajiwa kurejea nyumbani leo hii Jumatatu mara tu
baada ya kukamilika kwa kazi hii ya makabidhiano.
Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais
Juni 02, 2014 Blantyre,
Malawi
No comments:
Post a Comment