Bodi ya Africa Tourism Promotion Centre, waandaaji wenye
dhima ya kikomo ya kuratibu na kuendesha tamasha la Dunia la Utalii la “WORLD
GREAT SAFARITOUR” 2014/2015 ,wakishirikiana na kampuni ya Miss Tourism Tanzania
Beauty Pageant Limited, ipo mbioni kukamilisha mchakato wa kuteua nchi itakayo
kuwa wenyeji wa tamasha hilo la kimataifa la Utalii.
Katika hatua ya mwanzo mchakato huo ulishindanisha mabara
yote ya dunia,yakiwemo ya Asia,Ulaya,Marekani,Rusia, Asia,India na Afrika
, ambapo bara la Afrika liliyabwaga mabara mengine na kuteuliwa kuwa wenyeji wa
Tamasha hilo la Dunia.
Katika hatua ya pili waandaaji walishindanisha kanda za bara
la Afrika ,zikiwemo kanda za Afrika Magharibi,Afrika Kaskazini,Afrika ya Kati,
na Kusini ambapo Afrika Mashariki iliibuka washindi na kupewa heshima ya kuwa
wenyeji wa Tamasha hilo la Dunia la World Great Safari Tour 2014/2015.
Katika hatua ya mwisho ya mchakato wa kupata wenyeji wa
tamasha hilo, nchi za kanda ya Afrika ya Mashariki zinashindanishwa ambapo nchi
itakayo shinda kati ya Kenya,Burundi,Rwanda,Tanzania na Uganda ndiyo itakayo
pewa heshima ya kuwa wenyeji wa Tamasha hilo kubwa la kimataifa la Utalii
Duniani.
Hii itakuwa ni fulsa ya pekee kwa nchi itakayo pewa heshima
na hadhi hiyo kujitangaza kimatifa kiuchumi,kijamii na kubwa zaidi ni kutangaza
Vivutio vyake vya Utalii,Mianya ya Uwekezaji na Fulsa ilizo nazo za
ushirikiano wa kimataifa, lakini pia utengamano wa amani na usalama kwa raia na
wageni.
Aidha nchi itakayo shinda uenyeji huo, itapata fulsa ya
kuhamasisha vita dhidi ya Ujangili na Uharibifu wa Mazingira mkuithibitishia na
kuionyesha jumuiya ya kimataifa na kitaifa Juhudi ambazo serikali ya nchi
husika na mamlaka zake inafanya katika kupiga vita Ujangili na Uharibifu
wa Mazingira ,ikiwemo Uwindaji Haramu wa Misitu na Uharibifu wa Mzingira
yakiwemo ya Hifadhi Bahari na Nchi kavu.
Tamasha hilo ambalo litaonyeshwa moja kwa moja (LIVE)
duniani kote kupitia Televisheni na Mitandao ya Internet , litajumuisha zaidi
ya nchi 120, na kuangaliwa LIVE na zaidi ya watazamaji 1bilioni wa Telvisheni
na Mitandao ya Interneti.
Tamasha hilo Kuu la Utalii la Dunia “World Great Safari Tour
2014/2015” litajumuisha mashindano ya dunia ya Miss Tourism University World
2014/15,Mbio za nyika za Dunia za Ant Poaching International Marathon,
Wild Life International Marathon, National Parks International Marathon, Mbio
za kimataifa za Magari na Baisikeli na tuzo za Dunia za Utalii “World Tourism
Awaards 2014/2015”.
Pia kutakuwa na michezo mbalimbali ya viwanjani,majukwaani
,ufukweni na katika maeneo mengine ya kitalii na utalii ikiwemo masumbwi na
kubwa zaidi ni washiriki wote wa kitaifa na kimataifa kushiriki katika Safari
kuu ya kitalii ,wakiambatana na waandihi wa habari wa kimataifa na kitaifa wa
Televisheni,Video, Majarida na Magazeti katika vivutio vya Utalii,maeneo ya
kitamaduni na kihistoria vya nchi wenyeji.
Vigezo ambavyo Bodi intazingatia katika kuteua nchi wenyeji
ni pamoja na Uwepo wa Vivutio vya Utalii katika nchi husika, Dhamila na juhudi
za nchi husika kutangaza utalii wake kimataifa na kitaifa, Haja,Juhudi,Utayali
na dhamira ya kupiga vita Ujangili ,Uharibifu wa Mazingira ya nchi husika
katika nchi husika, lakini kubwa zaidi ni Amani,Usalama,Fulsa za Uwekezaji wa
kitalii na utengamano wa kimataifa na kitaifa wan chi husika.
Pia nchi kuwa na
uwezo wa kuwa wenyeji wa tukio au tamasha la kimataifa hapa suala la miundombinu
ya mawasiliano,usafiri,mahoteli,rasilimali watu,utayari wa serikali na mamlaka
zake za utalii,mazingira katika kushirikiana na waandaaji na mahitaji mengine
ya msingi vinazingatiwa.
Imetolewa na:
Gideon Erasto Chipungahelo
Makamu wa Rais Dunia Africa Tourism Promotion Centre/ Miss
Tourism Organisation
No comments:
Post a Comment