·Kiingilio ni kama mwaka jana, Banda maalumu kuitangaza
Tanzania
·Nchi 31 kushishiriki, zipo pia Wizara na Taasisi za
Serikali, Mashirika na Makapuni binafsi.
Na Johary Kachwamba- MAELEZO
Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam
(38th DITF) yanatarajia kuanza tarehe 28 mwezi huu na kufikia
kilele chake tarehe 8 Julai 2014 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu
J.K. Nyerere, barabara ya kilwa, jijini Dar-es-salaam.
Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade
Bibi. Jacqueline Mneney Maleko (pichani), imeeleza kuwa maonesho ya mwaka huu
yataongozwa na kauli mbiu isemayo “Tunaunganisha Uzalishaji na Masoko”
Amesema kuwa Kauli Mbiu hiyo imechaguliwa kutumika kuonesha
uhusiano uliopo kati ya Uzalishaji na Masoko na umuhimu wa mnyororo wa
uzalishaji ambao ndio chimbuko la upatikanaji wa Bidhaa bora zenye ushindani
katika soko.
Bibi. Maleko
amesema kuwa mwaka huu TanTrade imetenga eneo kubwa zaidi kwa ajili ya
Wazalishaji wa ndani ya nchi na kubainisha maeneo yatakayotumiwa na wazalishaji
hao kuwa ni jengo namba C.19 na eneo la wazi lililo nyuma ya ofisi za
Mkurugenzi wa Utafiti, Mipango na Uwezeshaji kwa ajili ya bidhaa za kilimo na
bidhaa zinazotengenezwa Tanzania.
Kuhusu ushiriki wa mataifa mengine katika maonesho hayo
amefafanua kuwa tayari nchi 31 zimethibitisha kushiriki maonesho hayo zikiwemo
Afrika Kusini,Czech Republic, China, Ghana, Indonesia, India, Iran, Finland,
Ugiriki, Italia, Japan, Jordan, Kenya, Korea ya Kusini, Malaysia, Marekani,
Misri, na Ujerumani.
Nchi zingine ni pamoja na Nigeria, Pakstani, Rwanda, Saudi
Arabia, Singapore, Sudani, Syria, Uganda, Uingereza, Burundi, Sweden, Vietnam
na Zimbabwe.
Aidha,
amefafanua kuwa makampuni ya nje 490 yamethibitisha kushiriki katika maonesho
hayo huku Wizara na Taasisi za Serikali zilizothibitisha kushiriki
maonesho hayo zikifikia 61.
Kwa upande wa
Mikoa amesema tayari mikoa 10 imethibitisha kushiriki ikiwemo, Mikoa ya Iringa,
Ruvuma, Mbeya, Pwani, Kigoma, Kagera, Geita, Mara, Manyara na Ruvuma.
Jumla ya Washiriki waliothibitisha kushiriki kutoka ndani ya nchi ni 1700.
Kuhusu
kiingilio wakati wa maonesho hayo amesema watu wazima walipia Shilingi
2,500 na watoto ni 500 kila siku kwa siku zote za maonesho isipokuwa tarehe 7
Julai,2014 ambapo ada itakuwa Shs. 3,000/= kwa watu wazima na watoto ni
Shs.1000/=
No comments:
Post a Comment