Tangazo

June 23, 2014

Twanga Pepeta yaupamba Uzinduzi wa Filamu mpya ya 'I Love Mwanza'

Mdau Richard Kasesela akionyesha umahiri wake wa kupiga tumba wakati bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ ilipotumbuiza katika hafla ya uzinduzi wa filamu mpya ya ‘I love Mwanza’, uliofanyika katika Hoteli ya JB Belmont jijini Mwanza Jumamosi usiku. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (hayupo pichani), ndiye aliyezindua filamu hiyo. PICHA ZOTE NA JOHN BADI
Badi Bakule akiimba.
Uzinduzi siku ya pili Jumapili ulifanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo, na Twanga Pepeta waliendelea kulishambulia jukwaa.
Kiongozi wa Twanga Pepeta, Luiza Mbutu akiongoza jahazi kukonga nyoyo za mashabiki ndani ya Jiji la Mwanza.

No comments: