- Norway kujirudishia misaada yake yote
nchini kupitia mkataba huu
Zitto Kabwe, Mb
Mkataba wa mgawanyo wa mapato yanayotokana na uzalishaji
wa Gesi Asilia (PSA) kati ya Shirika la Mafuta Tanzania na Kampuni ya Mafuta ya
Norway umevujishwa (https://onedrive.live.com/ view.aspx?cid= 0EC42B180C06D0B8&resid= EC42B180C06D0B8%21107&app= WordPdf).Toka
Mkataba huo uvuje na kuanza mijadala kwenye mitandao ya kijamii, habari zake
zimekuwa zinazimwa na hivyo kukosa kabisa mjadala mpana kitaifa na hasa kwa wananchi
wenye rasilimali zao. Mwanzoni wengi wetu tulidhani (kwa makosa) kuwa tatizo la
mkataba huu ni eneo la umiliki wa kampuni tu (shareholding) kulingana na namna
ulivyowasilishwa, kumbe mgawanyo mzima wa mapato unakwenda kinyume na maelezo
ya Serikali na TPDC kwa umma.
Mkataba uliovuja unaonyesha kwamba makubaliano ambayo
Serikali imeingia na Wawekezaji hawa kutoka Norway yanaenda kinyume kabisa na
mfano wa mkataba unaotakiwa kusainiwa (Model PSA). Kwa mujibu wa makala
iliyoandikwa na jarida la mtandaoni ( http://africanarguments.org/ 2014/07/04/leaked-agreement- shows-tanzania-may-not-get-a- good-deal-for-gas-by-ben- taylor/ )
Tanzania itapoteza zaidi ya shilingi 1.6 trilioni kila mwaka kulingana na
viwango vya uzalishaji wa gesi asilia katika Kitalu namba 2. Kitalu hiki
kinamilikiwa na Kampuni ya StatOil ya Norway na kampuni ya ExxonMobil ya
Marekani. Norway ni nchi inayosifika duniani kwa kupambana na rushwa na kwa
kutumia vizuri rasilimali yake ya mafuta.
Uchambuzi nilioufanya kulingana na viwango vya mgawo
wa mapato kati ya ‘model’ PSA na mkataba huu unaonyesha kwamba Tanzania itapata
mgawo kiduchu sana na kinyume na mgawo unavyopaswa kuwa. Mgawanyo ni kama ifuatavyo katika majedwali hapa chini; Ikumbukwe
kuwa mgawanyo huu hupatikana baada ya mwekezaji kuondoa gharama zake za
uzalishaji, kinachobakia ndio hugawanywa kati ya mwekezaji na Tanzania.
Jedwali 1 Mkataba wa mgawanyo wa Mapato unaopaswa kutumiwa
na TPDC (Model PSA) katika Mikataba na Wawekezaji
Viwango vya uzalishaji kila siku (MMscf per Day)
|
Mgawo wa TPDC (Profit Gas)
|
Mgawo wa Mwekezaji (Profit Gas)
|
|
0
|
249.999
|
50
|
50
|
250
|
499.999
|
55
|
45
|
500
|
749.999
|
60
|
40
|
750
|
999.999
|
65
|
35
|
1000
|
1249.999
|
70
|
30
|
1250
|
1499.999
|
75
|
25
|
1500
|
Above
1500
|
80
|
20
|
Jedwali 2 Mkataba wa mgawanyo wa Mapato kati ya TPDC
na Statoil/ExxonMobil.
Viwango vya uzalishaji kila siku (MMscf per Day)
|
Mgawo wa TPDC (Profit Gas)
|
Mgawo wa Mwekezaji (Share of Profit Gas)
|
|
0
|
299.999
|
30
|
70
|
300
|
599.999
|
35
|
65
|
600
|
899.999
|
37.5
|
62.5
|
900
|
119.999
|
40
|
60
|
1200
|
1499.999
|
45
|
55
|
1500
|
Above
1500
|
50
|
50
|
Ukilinganisha majdwali haya utaona kwamba mgawanyo wa
mapato utafaidisha zaidi kampuni ya StatOil na ni kinyume kabisa na mkataba
unavyopaswa kuwa.
Wakati mgawo wa nusu kwa nusu upo katika uzalishaji wa
chini kabisa kwenye ‘model PSA’, kwenye mkataba wa StatOil mgawo huo upo kwenye
uzalishaji wa juu kabisa. Ukilinganisha mgawanyo huu wa mapato, iwapo kiwango
cha ‘model PSA’ kingetumika Tanzania ingepata shilingi 1.6 trilioni zaidi ya
kiwango itakachopata kwenye mkataba wa sasa uliovujishwa. Hii ni kutokana na
Bei ambazo Shirika la Fedha la Kimataifa limeweka katika uchambuzi wake (https://www.imf.org/external/ pubs/ft/scr/2014/cr14121.pdf
) kuhusu Gesi asilia ya Tanzania.
Kwa mujibu wa Mwandishi Ben Taylor katika makala
iliyotajwa hapo juu, kiwango cha mapato ambacho Kampuni ya StatOil ya Norway
itajipatia kutokana na mkataba huu wa kinyonyaji, katika kipindi cha miaka 15
ya kuzalisha Gesi Asilia nchini itakuwa ni sawa sawa na misaada yote ambayo
Tanzania imepata kutoka Norway toka Tanzania ipate uhuru wake mwaka 1961.
Tangu Tanzania ipate Uhuru Norway imetoa
misaada ya thamani ya $2.5 bilioni, wakati kwa mkataba huu na Kampuni ya
StatOil ambayo inamilikiwa na Serikali ya Norway, kwa miaka 15 watapata $5.6
bilioni. Kwa hiyo kwa miaka 7 tu Norway itakuwa imerudisha misaada yote yake
mara mbili zaidi!
Kuvuja
kwa Mkataba huu kumesaidia sana kuona ukweli wa matamko ya viongozi wetu kuhusu
ni namna gani Tanzania itafaidika na utajiri wake wa gesi. Kama kwa mkataba huu
mmoja tu Taifa litapoteza matrilioni ya fedha kiasi hiki, ipoje hiyo mikataba
mingine 29? Hivi sasa ugunduzi wa Gesi Asilia nchini ni lita za ujazo trilioni
51 ambayo ni sawa na mapipa bilioni 10 ya Mafuta.
Katika Gesi Asilia yote
iliyopatikana nchini, StatOil peke yao wana jumla ya lita za uzajo trilioni 20,
sawa sawa na mapipa ya mafuta bilioni 4 (zaidi ya mafuta yaliyogunduliwa nchini
Uganda na Ghana kwa pamoja). Hata hivyo utajiri wote huu utainufaisha zaidi
Norway na Marekani kupitia makampuni yao kuliko watu wa Tanzania. Watanzania
watabakia wanapewa misaada ya vyandarua na mataifa haya ilhali wanafaidi Gesi
Asilia yetu.
Natoa
wito kwa Wizara ya Nishati na Madini kutoa tamko kuhusu mkataba huu kati ya
Shirika la TPDC na StatOil. Vile vile Kampuni hii ya StatOil kutoka nchi rafiki
mkubwa wa Tanzania ina wajibu wa kutoa maelezo ya kina kuhusiana na mkataba
huu. Serikali ieleze ni hatua gani inachukua kurekebisha Mkataba huu. StatOil
nao waeleze watachukua hatua gani kuhakikisha wanaacha unyonyaji huu mkubwa na
wa aibu kwa Taifa la Norway.
Sasa
ni wakati mwafaka Watanzania kuweza kuona mikataba yote ya Gesi na Mafuta
ambayo Serikali imeingia na Wawekezaji. Uwazi wa Mikataba sasa. Nimewahi
kuandika huko nyuma (PRESS RELEASE: Contracts review is a publicity stunt and creation of unnecessary uncertainty in the sector
) kwamba njia pekee ya Watanzania kufaidika na utajiri wa rasilimali zao ni
kuhimiza uwazi wa Mikataba. Mkataba huu wa StatOil uliovujishwa uwe ni chachu
ya kulazimisha Serikali na Makampuni kuweka mikataba yao wazi. Tuanze
mashinikizo haya sasa kwa faida ya vizazi vijavyo.
No comments:
Post a Comment