Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya
Jamii (NSSF), Crescentius Magori (kulia), na Mkuu wa Mahusiano wa NSSF, Eunice Chiume (kushoto), wakijadiliana jambo
na Golikipa namari moja wa Yanga, Juma Kaseja mara baada ya semina hiyo.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dar es Salaam
KLABU ya Yanga imeingia makubaliano ya kununua nyumba za Shirika la
Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa ajili ya wachezaji wake kupitia program maalumu.
Akizungumza katika hafla ya utiaji saini makubalinao hayo iliyofanyika
jana katika Hoteli ya Serena, Mkurugenzi wa Huduma na Uendeshaji wa NSSF,
Crecentius Magori alisema wachezaji wanapaswa kuona fahari kumiliki nyuma au
ardhi mjini, si magari.
Magori alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wachezaji wa Yanga ambao
walikuwepo katika utiaji wa saini makubaliano hayo, kuchangamkia mradi huo
uliopo makao mapya katika Kijiji cha Dege, Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
“Sisi tuko tayari kuwapa fomu na kwenda kuwaonyesha nyumba hizo za kisasa
zaidi, hivyo ningependa kuwashauri mpatapo fedha za mikataba, mkitoa kiasi nanyi
muwe wamiliki wa nyumba hizo.
“Kama utamudu na kutoa kiasi cha sh. mil.8 na kulipa kwa miezi mitatu
mfululizo, NSSF watawapa ufunguo na kuendelea kulipa kila mwisho wa mwezi kwa
miaka 15, kisha unakuwa mmiliki halali wa nyumba hiyo,” alisema Magori.
Aliongeza kuwa hata ikitokea mchezaji akafariki dunia, nyumba hiyo
itaendelea kuwa mali ya familia ya mhusika kwani itakuwa imerithiwa huku
akisihi wachezaji ambao si wanachama wa
NSSF, kujiunga ili kupata manufaa ya shirika hilo.
Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, alisema
makubaliano hayo ni matokeo ya mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa klabu hiyo,
Yusuf Manji na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhan Dau.
Alisema lengo ni kuhakikisha kila mchezaji wa timu hiyo anawezeshwa
kumiliki nyumba ikiwa ni moja ya mali ya kudumu ambayo itakuwa na manufaa yake
wakati anacheza, hata baada ya kustaafu soka.
|
No comments:
Post a Comment