Meneja Uhusiano wa
Airtel Tanzania Jackson Mmbando (kulia), akiteta na Katibu Mkuu wa TFF Selestine
Mwesigwa (wa pili kushoto), wakati wa semina elekezi ya Airtel Rising Stars iliyofanyika uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF
Salum Madadi na Mwenyekiti wa DRFA Almasi Kasongo.
==========
-========== -========
Katibu Mkuu wa
shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) Selestine Mwesigwa amesisitiza
umuhimu wa programu za vijana kwa maendeleo ya soka nchini na kuitaka kampuni
ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kuangalia uwezekano wa kuwa wadhamini wa
timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20.
Akifungua semina
elekezi kwa makatibu wakuu wa mikoa inayoshiriki mashindano ya vijana ya Airtel
Rising Stars (ARS) iliyofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumamosi
Julai 19, 2014 Mwesigwa alisema hali halisi inaonyesha kwamba miaka michache
ijayo wachezaji wengi watakaounda timu ya taifa ya U-20 watatokana na ARS hivyo
ni vema kampuni ya Airtel ikawa mdhamini mkuu wa timu hiyo.
Alisema kuwa suala
la programu za vijana ni agenda namba moja ya TFF na kuzitaka timu za ligi kuu
kuzingatia maagizo ya shirikisho hilo la kuwa na timu za vijana. “Klabu ya
Simba imefanikiwa sana katika suala hili na ni vema timu nyingine za ligi kuu
zikaiga mfano huo”, alisema Mwesigwa na kuipongeza Airtel kwa kuwekeza katika
soka la vijana.
“Wachezaji
wanapolelewa na klabu tangu wakiwa wadogo inakuwa ni rahisi kwao kuendana na
maadili ya klabu hiyvo kuwa na wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu tofauti
na wachezaji waosajiliwa kutoka sehemu mbali mbali wakiwa na umri mkubwa”,
alisema.
Aliwataka makatibu
hao wa mikoa kuzingatia kanuni ikiwa ni pamoja na umri ili kuwafanya vijana
watakaoshiriki mashindano ya Airtel Rising Stars kuwa na ushindani ulio sawa.
Mashindano ya ARS yanashirikisha vijana chini ya umri wa miaka 17.
Mwesigwa aliungwa
mkono na Mwenyekiti wa kamati ya vijana ya TFF Ayoub Nyenzi aliyesema kuwa
programu za vijana e.g. ARS ndiyo mkombozi wa kweli wa soka popete pale
duniani.
Mashindano
hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi katika ngazi ya mkoa Julai 27 na
kushirikisha mikoa ya Mbeya, Morogoro, Mwanza, Ilala, Kinondoni na Temeke kwa
upande wa wavulana huku timu za wasichana zikitoka mikoa ya Mwanza, Mbeya,
Zanzibar, Ilala, Kinondoni na Temeke.
Akiongea katika
semina hiyo Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando aliwapongeza
viongozi wa mikoa kwa kazi nzuri iliyoiwezesha Tanzania kutwaa ubingwa wa
mashindano ya kimataifa ya ARS (wasichana) yaliyofanyika Nigeria na kuzawadiwa
USD 10,000, medali na vikombe.
“Vile vile timu ya
wavulana ilifanya vizuri sana na ni imani yangu kwamba mwaka huu Tanzania
itashinda vikombe kwa wasichana na wavulana”, alisema na kusisitiza nia thabiti
ya Airtel kuendelea kuboresha mashindano hayo.
Naye Mkurugenzi wa
Ufundi wa TFF Salum Madadi aliwataka makatibu hao kufanyakazi kwa karibu na
kamati ya vijana ya TFF inayosimamia mashindano hayo.
No comments:
Post a Comment