Tangazo

September 26, 2011

Morogoro yaibuka kidedea katika Michuano ya Airtel Rising Stars

Mwamuzi Bora wa michuano ya kukuza vipaji vya soka kwa vijana ya Airtel Rising Stars, Baraka Rashid akiwa na tuzo yake baada ya kukabidhiwa katika kilele cha michuano hiyo, Jumamosi Septemba 24, kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Golikipa Bora wa michuano ya kukuza vipaji vya soka kwa vijana ya Airtel Rising Stars, Denis Richard wa Mkoa wa Dar es Salaam, akikabidhiwa zawadi ya kikombe na Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya simu ya Airtel, Jane Matimbe katika kilele cha michuano hiyo. Fainali za michuano hiyo ilishirikisha timu nne za mikoa ya Morogoro, Iringa, Mwanza na Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Airtel, Rahma Mwapachu (kushoto) akimkabidhi zawadi ya kikombe, mchezaji bora wa michuano ya kukuza vipaji vya soka kwa vijana ya Airtel Rising Stars, Samil Omar wa timu ya Mkoa wa Mwanza.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Leonald Thadeo (kulia), akimkabidhi nahodha wa timu ya kombaini ya vijana wa sekondari za Mkoa wa Morogoro, Charles John  kombe la ubingwa wa michuano ya kukuza vipaji vya soka kwa vijana ya Airtel Rising Stars, katika kilele cha michuano hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam juzi .Katika fainali hiyo Morogoro iliyoongoza kwa pointi ilitoka sare ya bao 1-1 na Dar es Salaam.
Wachezaji sita bora waliochaguliwa katika michuano ya kukuza vipaji vya soka kwa vijana ya Airtel Rising Stars, wakiwa na vyeti vyao baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi. Wachezaji hao watashiriki kliniki ya Manchester United itakayofanyika Uwanja wa Taifa kuanzia Oktoba 30 hadi Novemba 2, mwaka huu. Wachezaji wengine watatoka Kenya, Siera Leon na Malawi.

No comments: