Tangazo

October 7, 2014

Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani watembelea Kiwanda cha TBL Arusha

 Mratibu wa Usalama afya na mazingira mahali pa kazi wa Kiwanda cha Bia nchini TBL Arusha Heavy Kassena akiwaonyesha baadhi ya maeneo na shughuli zinazofanywa kiwandani hapo askari wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Arusha, pembeni yake ni Ofisa Uhusiano wa TBL Makao Makuu Dorris Malulu, wakati wa ziara iliyofanyika kiwandani hapo juzi.

 Mratibu wa Usalama afya na mazingira mahali pa kazi wa Kiwanda cha Bia nchini TBL Arusha Heavy Kassena akiwaonyesha shughuli zinazofanywa kiwandani hapo baadhi ya askari wa kikosi cha Usalama barabarani mkoa wa Arusha waliotembelea kiwandani hapo juzi.
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Arusha Marrison Mwakyoma akitembelea kiwanda cha Bia TBL Arusha wakati wa ziara ya askari wa usalama barabarani waliotembelea kiwandani hapo hivi karibuni kwa lengo la kuimarisha uhusiano wa kikazi.
 Mtaalamu wa upishi wa Bia katika Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) kilichopo mkoani Arusha Jacob Mgome akiwapa maelezo askari wa kikosi cha usalama barabarani waliotembelea kiwandani hapo juzi
 Mtaalamu wa upishi wa Bia katika Kiwanda cha Bia Tanzania (TBL) kilichopo mkoani Arusha Jacob Mgome akiwapa maelezo askari wa kikosi cha usalama barabarani namna Shayiri inavyopokelewa kiwandani hapo wakati wa ziara ya askari hao
 Mtaalamu wa kitengo cha kutibu maji yanayotumika kiwandani hapo akiwapa maelezo askari wa usalama barabarani namna maji hayo yanavyosafishwa na kisha kurejea tena kiwandani hapo kwa ajili ya kumwagilia bustani wakati wa ziara ya maofisa hao juzi.
 Askari wa usalama barabarani mkoa wa Arusha wakiwa ndani ya kiwanda cha Bia kilichopo Arusha wakati wa ziara yao ya kikazi ya kutembelea kiwanda hicho juzi.


 Mtaalamu wa upishi wa Bia katika Kiwanda cha Bia (TBL), Arusha Jacob Mgome akiwaonyesha askari wa usalama barabarani waliotembelea kiwandani hapo namna maji yanaytotumika kupikia Bia yanavyopitishwa.
Askari wa Ulinzi katika kiwanda cha TBL Arusha akiwaonyesha namna kifaa maalumu cha kupimia kilevi kwa askari wa usalama barabarani walipofanya ziara yao ya kikazi kiwandani hapo juzi.

1 comment:

Boneka Full Body said...

thanks for sharing