Tangazo

October 20, 2014

HOTEL ZA DOUBLE TREE BY HILTON TANZANIA WADHAMINI SIKU YA CHAKULA ILIYOFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA TANGANYIKA INTERNATIONAL SCHOOLS

 Hotel Za Double Tree By Hilton Tanzania Tarehe 18.10.2014 walidhamini Siku Ya Maonesho Ya chakula Iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Tanganyika International Schools.

Akielezea Madhumuni ya kuandaa siku hiyo  Mkurugenzi wa Mauzo  wa Hotel za Double Tree By Hilton Tanzania Bwana Florenso Kirambata alisema kuwa nia yao kubwa ni kuweza kuyapa fursa makampuni mbali mbali na wajasiliamali wadogo wadogo kuweza kuonyesha uwezo wao na bidhaa wanazotengeneza.

Mr Florenso  akaongeza kuwa zaidi ya wajasiriamali wadogo wadogo 100(mia Moja) na Wakubwa 50(hamsini) walishiriki kwenye maonesho hayo hasa lengo kuu ikiwa ni kuonesha aina mbali mbali za vyakula wanavyozalisha hivyo kuweza kujitangaza na kufahamika.

Pichani Juu Katikati ni Meneja Masoko wa Hotel za Double Tree By Hilton Bwana Florenso Kirambata kushoto ni mpishi mkuu wa Double Tree Hassan na kulia ni Ayman.
 Mpishi Msaidizi wa Hotel ya Double Tree  Awadh(kushoto) Akiwa Anapata maelekezo toka kwa Mpishi mwenzake Ayman namna ya kuandaa na kuchanganya vyakula

  Mpishi mkuu wa Hotel za Double tree Bwana Hassan akitoa maelekezo kwa wasaidizi wake 
 Meneja Masoko wa Hotel za Double Tree By Hilton Bwana Florenso Kirambata akiwa na wapishi wa Hotel za Double Tree wakipata maelekezo kwa mmoja wa washiriki wa Maonesho ya chakula
 Wapish wa Hotel Za Double Tree Wakiangali moja ya Bidhaa Toka kwa mshiriki wa maonesho ya siku ya chakula
 Mwaandaaji mku wa Maonesho hayo wa kwanza Kulia akiwapa maelekezo wapishi wa Hotel za Double Tree 
 Mpishi msaidizi wa Hotel za Double Tree akiwapa maelekezo wateja waliotembelea banda lao namna chakula cha Hot Dog kinavyotengenezwa
 Banda la American Garden Walikuwepo nao kuonyesha Bidhaa zao Tofauti tofauti
 Watu mbali mbali wakiendelea kutembelea mbanda tofauti tofauti  na kujionea bidhaa
 Waudhuriaji wakiendelea kupata vyakula na kufarihia ladha tofauti za vyakula
 Wahudhuriaji pia walipata nafasi ya kubadilishana mawazo
 Wahudhuliaji wakiendelea kupata ladha tofauti za vyakula.

No comments: