Simu ya Upepo : “N
G O M E” Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM
22150463 Sanduku la
Posta 9203,
Tele Fax : 2153426
Barua pepe
: ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti : www.tpdf.mil.tz
Taarifa ya Kifo
Jeshi la Ulinzi
la Wananchiwa Tanzania (TWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha Brigedia Jenerali (mstaafu) Hashimu Said Mtezo kilichotokea tarehe
04 Oct 14 kwa ugonjwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo Dar es Salaam
alipokuwa akipata matibabu.
Alizaliwa Machi
18, 1945 Wilaya ya Dodoma Mjini na alisoma katika shule ya Sekondari ya Tabora
kuanzia mwaka 1962 hadi alipohitimu Kidato cha Sita mwaka 1967. Alijiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania
tarehe 20 Juni, 1968. AlitunukiwaKamisheniJuni 05,1969.
Katika utumishi
wake Jeshini, alihudhuria na kufaulu kozi mbalimbali ndani na nje ya nchi. Marehemu Brigedia Jenerali Mtezo amewahi kushika
madaraka mbalimbali, Mwambata Jeshi nchini Zimbabwe 1987 hadi 1993, Mkurungenzi
wa Mafunzo Makao Makuu ya JWTZ 1993 hadi 2002.
Hadi anafariki alikuwa amestaafu Juni 30,
2002 baada ya kulitumikia Jeshi kwa muda wa miaka 34. Mazishi yatafanyika tarehe
07 Octoba, 2014 Mbezi Lous.
MUNGU AILAZE
MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU BRIGEDIA JENERALI HASHIMU SAIDI MTEZO
(MSTAAFU) AMINA
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari naMahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P 9203, Dar es Salaam, Tanzania.
KwaMawasiliano zaidi: 0783 - 309963
No comments:
Post a Comment