Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali
Dr. Servacius Likwelile akielezea mikakati ya nchi ya Tanzania katika kuinua
uchumi na kuongeza pato la Taifa kwenye Mkutano uliofanyika leo juu
yuliohusu masuala na fedha na sera ya
kiwango cha ubalilishaji fedha.PICHA KWA HISANI YA WIZARA YA FEDHA
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
BENKI
YA DUNIA NA IMF YAANZA MIKUTANO YA MWAKA
MJINI WASHINGTON DC - MAREKANI
Kila mwaka Bodi ya
Magavana ya Shirika la Fedha la Kimataifa na kundi la Benki ya Dunia hukutana
kwa ajili ya kujadili kazi za Taasisi
zinazowahusu. Mikutano hii imeanza tarehe 06 Octoba na itafikia kilele chake
hapo tarehe 13, mwezi Octoba, 2014.Mikutano hii hufanyika mjini Washington DC
kwa miaka miwili mfululizo na kwa mwaka wa tatu hufanyika kwa nchi
mwanachama.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali
Dr. Servacius Likwelile ndiye kiongozi wa ujumbe kutoka Tanzania na yeye
anawakilisha kama Gavana mbadala (Alternate Governor) pamoja na Gavana wa Benki
Kuu Prof. Benno Ndulu ambaye pia ni Gavana katika mikutano hii.
Mikutano hii inatoa
nafasi ya kuweza kujadiliana na Benki ya Dunia pamoja na Shirika la Fedha la
Kimataifa kuhusiana na hali ya uchumi kwa maana ya sera za fedha na sera za
mapato na matumizi. Nia yao kubwa ni kutaka kusikia mawazo yetu kuhusu jinsi ya
kuboresha uchumi ili wawe katika nafasi nzuri ya kuangalia ni wapi wanaweza
kutusaidia kuboresha na kuona kwamba nchi yetu inaendelea kufanya vizuri zaidi.
Maeneo ambayo yameshajadiliwa ni pamoja sera kuhusu kiasi cha ubadilishaji
fedha, mapato ya nchi kwa ujumla na mwendo wa matumizi ya fedha.
Hali ya utendaji wa kiuchumi na hali ya matumizi na
mapato ya fedha ya Tanzania imeonekana ni ya kuridhisha japo pado kunachangamoto ya ajira.
Hali ya hewa mjini
hapa ni baridi kiasi na manyunyu ya hapa na pale.
Imetolewa na:
Ingiahedi
Mduma
Msemaji -Wizara ya Fedha
Washington
D.C
7/10/2014
|
No comments:
Post a Comment