|
Meneja uhusiano wa airtel Jackson Mmbando akizindua na kutangaza
rasmi namba itakayowawezesha watanzania
kushiriki mashindano ya kusaka vipaji ya muziki ya airtel trace music star kwa kukerekodi
na kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi jana
|
|
Balozi wa airtel music stars Tanzania Ommy Dimpos akitangaza
rasmi namba itakayowawezesha watanzania
kushiriki mashindano ya kusaka vipaji ya muziki ya airtel trace music star kwa
kukerekodi na kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi jana Coco beach.
|
|
Mmoja kati ya wasanii
waliojitokeza akijaribu kuimba
kwenye namba maalum ya kushiriki mashindano ya Airtel Trace Music Stars katika
viwanja vya coco beach huku meneja uhusiano wa airtel Jackson Mmbando
akishuhudia. Airtel imezindua mashindano haya ya Airtel Trace Music stars kwa
lengo la kuwasaidia wasanii wanaochipukia nao kufikia malengo yao. |
|
Baadhi ya wasanii
waliojitokeza wakijaribu kuimba na kurekodi kwenye namba maalum ya kushiriki
mashindano ya airtel trace music stars katika viwanja vya coco beach ambapo
airtel ilimezindua rasmi namba ya kushirmaki shindano la airtel trace music
stars kwa lengo la kuwasaidia wasanii wanaochipukia nao kufikia malengo yao ya
kuwa nyota wa muziki.
|
|
Wasanii wa kundi la Yamoto band wakiwa na msanii maarufu
nchini ambae pia ni balazo wa airtel trace music stars tanzania Ommy Dimpos wakionyesha
namba maalum itakayotumika kupiga na kutuma nyimbo kwa wasanii chipukizi kwenye
shindano la airtel trace music stars lililozinduliwa rasmi jana.
|
|
Msanii wa kundi maarufu na linalofanya vizuri toka TMK Yamoto
band akionyesha vitu vyake.
|
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
* Piga simu namba 0901002233 Imba na Ushinde na Airtel Trace
Music Stars
KAMPUNI ya simu za mkononi ya airtel imezindua rasmi namba itakayowawezesha
watanzania kushiriki mashindano ya kusaka vipaji ya muziki ya Airtel Trace
Music Stars kwa kurekodi na kutuma nyimbo zao kwa kutumia simu zao za mkononi
huku baadhi ya wasanii chipukizi wakipata nafasi yakuonyesha vipaji vyao katika
viwanja vya Coco Beach.
Akizungumza katika uzinduzi huo uliopambwa na burudani
mbalimbali ikiwemo Yamoto bendi katika viwanja vya Coco Beach jijini Dar es Salaam,
Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw. Jackson Mmbando amesema kila mtanzania anayo
nafasi ya kushiriki katika shindano hilo
kwa kupiga
simu namba 0901002233.
Aidha Mmbando ameongeza kuwa lengo la kuanzisha shindano
hilo ni kuinua vipaji vya watanzania wenye kujua kuimba ili wapate nafasi ya kuwa
staa wa kimataifa.
Nae balozi wa shindano hilo Ommy Dimpoz amewaomba watanzania
kujitokeze kwa wingi katika kushiriki mashindano hayo ambapo mshindi atajinyakulia zawadi
kabambe ikiwemo kurekodi na kusambaziwa
nyimbo zake chini ya studio kubwa ulimwenguni pamoja na safari ya kwenda nchini
marekani kwa ajili ya kupata mafunzo ya kimuziki na nguli wa muziki wa Amerika Akon.
No comments:
Post a Comment