Balozi
Ndayiziga katika mojawapo ya warsha ya EAC hivi karibuni. Kulia ni
mtaalamu wa habari na mratibu wa mafunzo ya wandishi wa habari EAC, Bw.
Sukhdev Chhatbar.
Mkufunzi katika Mafunzo hayo,
Balozi Jeremy Ndayiziga (kushoto enzi za uhai wake) akimkabidhi cheti Mroki Mroki, kutoka
Father Kidevu Blog ambaye pia ni Mpigapicha wa Masuala ya Mtangamano wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa kushiriki kikamilifu mafunzo hayo ya masuala ya Mtengamano wa EAC.
Anaeshuhudia Katikati ni Elizabeth Wanyoike wa GIZ ambao walifadhili
mafunzo hayo na Jumuia ya Afrika Mashariki.
**********
Na
Mtua Salira, EANA
Mshauri Mtaalamu wa muda mrefu wa Masuala ya
Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Balozi Jeremy Ndayiziga (54)
amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi ugonjwa wa kisukari mjini
Bujumbura,Burundi.
Balozi
huyo raia wa Burundi kwa mujibu wa marafiki wa karibu na ndugu zake alifariki
Jumatano wiki iliyopita na anatarajiwa kuzikwa nchini Burundi Jumanne ijayo,
Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA) limeripoti.
Kutokana
na hali yake ya afya kuendelea kudorora, Balozi Ndayiziga alilazimika kukatwa
mguu wake wa kulia katika Hopsitali ya Nairobi kutokana kuzidiwa na
ugonjwa wa kisukari na hivyo kubaki hospitalini kwa miezi ipatayo minne. Afya
yake ilionekana kuimarika kidogo na alikuwa anakaribia kupona.
Mara
ya mwisho alionekana makao makuu ya EAC mjini Arusha, Tanzania katikati ya
Novemba mwaka huu katika mkutano wa Maofisa Mawasiliano wa EAC.
Jina
la Balozi Ndayiziga ni maarufu kwa watendaji wa EAC kutokana na umahiri wake wa
uchapaji kazi,uongozi wa busara na kuwa muumini wa itikadi ya Shirikisho la
EAC. Ndiye aliyeiongoza nchi yake katika harakati za kujiunga na EAC 2007.
‘’Marehemu
Balozi Ndayiziga alikuwa mtu maarufu, mchapakazi mwenzangu na kwa kweli, zaidi
ya yote alikuwa rafiki yangu wa karibu sana,’’ alisema Jean Rigi,Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afrika Mashariki nchini Burundi na kuongeza kuwa wengi
watamkosa na ni pigo kubwa kwa wote wanaopigania kujenga Afrika Mashariki na
raia wake.
Mkongwe
wa masuala ya habari nchini Tanzania Jenerali Ulimwengu kufuatia taarifa ya kifo
hicho alisema: ‘’Nimepata mshtuko mkubwa! Nilijua kwamba alikuwa anaugua lakini
nilifikiri kwamba ni jambo la kawaida tu linaloweza kudhibitiwa.Nimesikitishwa
sana kwa sababu alikuwa ni mtu makini na mwalimu mwenye uelewa wa hali ya juu
na alikuwa mwakilishi mzuri wa masuala ya mtangamano wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki.Nilifanya naye kazi kwa karibu sana kwa kipindi cha zaidi ya miaka
mitano.’’
Naye
mmoja kati wafanyakazi aliokuwa anafanya nao kazi kwa karibu ni Sukhdev
Chhatbar, Mtaalamu wa Masuala ya Habari, ambaye alielezea kusitishwa na kifo
Balozi Ndayiziga.
‘’Tulikuwa
tunawasiliana vyema katika uekelezaji wa miradi mbalimbali.Alikuwa mtu maarufu,
mwenye msimamo thabiti,mwenye busara na alikuwa tayari kufanya lolote
kuimarisha mchakato wa mtangamano wa kikanda,’’ alisema Chhatbar, mwandishi wa
habari maarufu aliyekuwa anasafiri na kusimamia miradi ya pamoja ya EAC na
marehemu Balozi huyo katika nchi wananchama wa jumuiya.
Marehemu
ameacha mjane na watoto wanne.
No comments:
Post a Comment