Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade, kushoto akiwa na afisa mtendaji mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na
maendeleo, Prof Mick Moore, wakiongoza majadiliano juu ya mada mbalimbali
zilizowasilishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi
na maendeleo,mkutano uliofanyika jana jijini Arusha
Wataalamu wa kimataifa
wa masuala ya kodi wakiendesha
mjadala katika mkutano wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa masuala
ya kodi,mkutano uliofanyika jana jijini Arusha ,Kamishna Msaidizi wa Mamlaka
ya Mapato Uganda (URA), Milly Nalukwago (kushoto), Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Rished Bade (katikati) na Mtaalam wa Kodi wa Uingereza, Rhiannon Mc Cluskey.
Kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA RISHED BADE
kushoto akiwa na afisa mtendaji mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na
maendeleo Prof MICK MOORE wakiongoza majadiliano juu ya mada mbalimbali
zilizowasilishwa katika mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi
na maendeleo,mkutano uliofanyika jana jijini Arusha
Mwakilishi wa Channel Ten Arusha, Jamila Omar (katikati) , Mwakilishi wa
kituo cha Star TV Arusha, Ramadhani Mvungi ,Iddy Uwesu wa Azam
tv Arusha wakifanya mahojiano maalumu na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Rished Bade jijini Arusha wakati wa
mkutano mkuu wa mwaka wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo.
***********
Mamlaka ya mapato nchini TRA imeanza kuchambua ripoti
ya utafiti uliofanywa na kituo cha kimataifa cha utafiti wa masuala ya kodi na maendeleo
inayobainisha changamoto mbalimbali za ulipaji kodi katika
maendeo mbalimbali nchini.
maendeo mbalimbali nchini.
Zoezi la uchambuzi wa ripoti hizo linatajwa kuwa
na shabaha ya kuangalia mapungufu yaliyopo na kuboresha mifumo ya sheria na ulipaji
kodi kwa hiari.
Sehemu ya Taarifa ya utafiti uliofanwa katika
kipindi cha mwaka uliopita na kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo katika mikoa mbalimbali nchini,
inabainisha mazingira tofauti ya ulipaji wa kodi ambapo baaadhi ya maeneo yameonekana kuwa katika changamoto kubwa za ukwepaji kodi.
Kamishana wa TRA Rished Bade kizungumza Jijini
Arusha wakati wa Mkutano wa kimataifa baina yao na kundi la wataalamu,
wanaofanya utafiti kuhusu masuala ya kodi duniani amesema pamoja na mapitio ya ripoti
za utafiti wa taasisi hiyo,fursa hiyo inatoa mwanya kwa wataalamu wa ndani
kujifunza mbinu za kushughulikia changamoto za walipa kodi wanaofanya biashara
za kimataifa.
Awali Afisa Mtendaji Mkuu wa kituo cha kimataifa cha kodi na maendeleo Profesa Mick Moore ameeleza kusudio la tafiti zao katika nchi mbalimbali za Afrika kuwa unalenga kuimarisha mifumo ya kodi hususani katika sekta za maliasili zikiwemo Madini,Gas na Mafuta.
Katika hatua nyingine Mamlaka ya mapato nchini
TRA imeibuka kinara kwa kuwa na hesabu bora miongoni mwa taasisi za serikali
kwa mwaka 2013-2014 zinazotolewa na bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu nchini
NBAA ambapo kamishna wa mamlaka hiyo akizungumza Jijini hapa katika hafla ya kukabidhiwa
ushindi huo amesema hatua hiyo inazidi kuwajengea imani walipa kodi juu ya
utendaji wa chombo hicho.
Raha tele tabu ya nini?:
zinaonyesha ongezeko la idadi ya walipa kodi chini,idadi iliyopo sasa inatajwa
kuwa ndogo kulinganisha na mataifa mengine kutokana na mfumo wa kibiashara usio
rasmi unaopelekea kupunguza idadi ya walipa kodi wanaofikia milioni moja nukta
nane hivi sasa.
No comments:
Post a Comment