Ofisa wa Kiwanda cha Bia TBL Arusha
aliyeo katika idara ya uzalishaji akiwaonyesha baadhi ya wanahabari wa Arusha
namna bia inavyohifadhiwa wakati wa ziara ya waandishi iliyokwenda sanjari na
zoezi la kuonja bia na kutembelea kiwanda hicho mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya waandishi wa habari wa
Arusha wakiangalia utunzaji wa mazingira unavyofanywa na Kiwanda cha Bia cha
Arusha (TBL), ambapo maji yote yanayotumika kwa shughuli za kiwandani hapo huhifadhiwa
na kuchunjwa kwa ajili ya matumizi mengine yakiwamo bustani na vyooni,
waandishi hao walitembelea kiwandani hapo kwa ajili ya kuongeza ufahamu zaidi
wa utunzaji mazingira.
Meneja Mpishi wa Kiwanda cha Bia TBL
Arusha Ben Mwanri akiwasilisha mada kwa wanahabari wa Arusha waliotembelea
kiwandani hapo kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali ikiwamo pia zoezi la
kuonja Bia lililowashiurikisha waandishi hao wa habari.
Afisa
Uhusiano wa Kampuni ya Bia nchini (TBL), Edith Mushi akiwapa maelekezo
kwa baadhi ya waandishi wa habari wa Arusha waliotembelea kiwandani hapo kwa
lengo la kuendelea kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho
kilichopo Arusha
:
Meneja wa Kiwanda cha Bia Arusha (TBL), Salvatory Rweyemamu akimkabidhi zawadi
mshindi wa kwanza wa zoezi la kuonja bia Deogratisu Moita aliyeibuka mshindi
wakati wa zoezi la kuonja bia lilolowashirikisha baadhi ya waandishi wa Arusha,
waandishi hao walifanya ziara yao kiwandani hapo hivi karibuni
Afisa wa Usalama Kiwanda cha Bia
(TBL) Arusha Heavy Kisena akiwaonyesha baadhi ya waandishi wa habari wa Arusha
namna mitambo wa kusafisha maji yanayotoka kiwandani unavyofanya kazi.
Waandishi hao walifanya ziara yao hivi karibuni kwa lengo la kujifunza zaidi
utunzaji wa mazingira
Afisa Usalama wa TBL Arusha Heavy Kisena
akiwatembeza waandishi wa habari wa Arusha katika maeneo mbalimbali ya kiwanda
hicho wakati wa ziara yao iliyofanyika hivi karibu
Tunaonja Bia: Baadhi ya waandishi wa habari wa
Arusha wakishiriki zoezi la kuonja bia lililofanyika kiwandani hapo wakati wa
ziara ya wanahabari kiwandani hapo hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment