Mkulima
toka mkoani Pwani Ramadhani Dilunga miaka 53 na Mwalimu mstaafu wa
Mtwara bw, Namtapika Kilumba (60) ni miongoni mwa Watanzania watatu
walioibuka washindi kwenye droo ya kwanza ya Airtel Yatosha Zaidi
iliyofanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Washindi
hao kila mmoja ameibuka mshindi wa gari aina ya IST Toyota mpya, ikiwa
ni siku chache tu tangu kuzindulia kwa promosheni hiyo.
Airtel
Tanzania wiki iliyopita ilitangaza dhamira yake ya kuwazawadia wateja
wake wanaojiunga na bando za Airtel Yatosha gari moja kila siku kwa
siku 60 ambapo mwishoni mwa wiki tayari magari matatu yalipata washindi.
Balozi
wa Airtel, na msanii maarufu wa filamu nchini, Elizabeth Michael
‘Lulu’, ndiye aliyekuwa na jukumu la kuwapigia simu washindi na kuwapa
taarifa hizo nzuri kwa mwaka 2015 chini ya Mkaguzi Mwandamizi kutoka
Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Bakari Maggid
Wa
kwanza kupigiwa alikuwa Namtapika Kilumba wa Mtwara mwenye umri wa miaka
60 na aliposikia sauti ya Lulu ikisema; “Ninapenda kukutaarifu kuwa
umeshinda gari aina ya IST Toyota mpya baada ya kujiunga na Airtel
Yatosha Zaidi”, alipiga kelele kwa furaha na mara moja akamshukuru Mungu
pamoja na Lulu.
“Mungu
wangu. Sikutarajia kabisa kama leo ningepata taarifa nzuri kama hizo!
Kumbe ni kweli kuwa mtu yeyote anaweza kushinda promosheni ya Airtel?
siamini,” alisema … kwa njia ya simu; na hata wengine pia waliopigiwa
simu na Lulu walikuwa na maoni yanayoshabihiana na hayo.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya droo hiyo, Meneja Uhusiano wa Airtel,
Jackson Mmbando, alisema: “Haya ndio kwanza magari matatu tu. Bado
mengine 57 yote aina ya IST Toyota mapya kabisa yapo ‘showroom’. Ndani
ya 60 za mwaka huu, wateja 60 wa Airtel watakuwa wakiishi maisha mapya
katika dunia ya ndoto zao.
“Watakuwa
ni wamiliki wa magari kwa kujiunga na bado za Airtel Yatosha zaidi kwa
kupiga simu *149*99# na kujiunga. Hebu fikiria, unapata muda wa maongezi
zaidi, vifurushi vya internet zaidi, SMS zaidi na bado unakuwa na
nafasi ya kujishindia gari.”
Mmbando
alimtaja mshindi mwingine kuwa ni Mwajabu Churian mwenye umri wa miaka
27 na mfanyabiashara anaeishi Mbagala huku akiwasihi wateja wa Airtel
kuendelea kufurahia huduma hiyo.
No comments:
Post a Comment