Tangazo

June 12, 2015

KOMREDI KINANA AUNGURUMA KARAGWE, ATEMBELEA KIWANDA CHA KAGERA SUGAR

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akishuka kutoka kwenye katapila baada kuliendesha wakati wa kazi ya kusawazisha shamba la kupanda miwa alipotembelea mashamba ya miwa ya Kiwanda cha Sukari cha Kagera, wilayani Misenyi, Kagera, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akishuka kutoka kwenye katapila baada kuliendesha wakati wa kazi ya kusawazisha shamba la kupanda miwa alipotembelea mashamba ya miwa ya Kiwanda cha Sukari cha Kagera, wilayani Misenyi, Kagera, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Komredi Kinana akiwa na Mkurugenzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kagera alipotoka kukagua mitambo ya kusukuma maji kwa ajili ya umwagiliaji katika mashamba ya miwa.
 Kikundi cha ngoma za asili cha Chanika, kikitumbuiza  wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili kuzungumza na wananchi katika Kijiji cha Kihanga, wilayani Karagwe, Kagera.
 Wananchi wa Kijiji cha Kihanga wakishangilia walipokuwa wakimlaki komredi Kinana kijijini hapo.
 Komredi Kinana akihutubia wananchi katika Kijiji cha Kihanga,
 Komredi Kinana akikagua mizinga ya nyuki alipotembelea mradi wa nyuki unaoendeshwa na vijana eneo la Kishovu, wilaani Karagwe leo.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya National Beekeeping Supplier ltd, Kaizerege Camara akimuonesha Komredi Kinana kifaa kinachotumika kufugia malkia wa nyuki katika mradi huo.
 Komredi Kinana akishiriki ujenzi wa banda la mradi wa kufugia nyuki katika mradi huo
 Makandarasi wa kampuni ya kichina ya Chicco, inayojenga barabara ya Kyaka-Bugene wilayani Karagwe, wakisalimianana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliyekwenda kukagua ujenzi huo eneo la Mugulakorongo, Ndama.
 Komredi Kinana akiangalia jinsi mitambo inayoweka lami nyepesi katika barabara hiyo ya Kyaka-Bugene

 Komredi Kinana akishiriki kupiga lipu chumba cha darasa katika Shule ya Msingi ya Katembe, Kata ya Kituntu, wilayani Karagwe/
 Komredi Kinana akitoka kushiriki ujenzi wa Kiwanda cha Kahawa na Maharaga cha Kadress eneo la Ndama, wilayani Karagwe, Kagera.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akishangiliwa na wananchi  katika Kijiji cha Nyakaiga, Kibondo, wilayani Karagwe,alipokuwa akuhutubia na kuwapiga vijembe wapinzani kwamba kamwe hawataweza kushinda uchaguzi mkuu na kuingia Ikulu.
 Komredi Kinana akihutubia katika Kijiji cha Nyakaiga, Kata ya Kibondo, wilayani Karagwe, Kagera
 Wananchi wa Kijiji cha Nyaishozi, Kata ya Nyaishozi wakishangilia baada ya Komredi Kinana kuwasili katika mkutano wa hadhara.
 Komredi Kinana akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa  Saccos ya Umoja wa Vijana wa CCM, Katanga mjini, wilayani Karagwe. Kulia ni Meneja wa Saccos hiyo,Majaliwa Said.
 Komredi Kinana akiwanyanyua mikono juu vijana waendesha Bodaboda watano  alipowakabidhi pikipiki za mkopo uliotolewa na Saccos hiyo.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano katika Mji wa Katanga, Makao Makuu ya Wilaya ya Karagwe. mkoani Kagera.
 Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Gozibeth Blandes akihutubia katika mkutano huo
 Komredi Kinana akiteta jambo na Nape wakati wa mkutano wa hadhara katika Mji wa Katanga, Karagwe.
 Komredi Kinana akihutubia wananchi katika Mji wa Katanga, Makao Makuu ya Wilaya ya Karagwe, mkoani Kagera.

No comments: