Tangazo

June 7, 2015

WAZIRI MEMBE AUTIKISA MJI WA LINDI, ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS WA TANZANIA

Mashabiki wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiwa wamejipamba kwa rangi mwilini katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa wa Lindi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akizungumza na wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa leo Juni 07.2015, wakati akitangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba.PICHA ZOTE/JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG
Makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakiwa na bango lenye ujumbe katika mkutano huo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Lindi. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoani humo, Mzee Ali Mtopa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kulia) na Mkewe Dorcas, wakijadilina jambo na Mzee Ali Mtopa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe akiusalimia umati wa wana CCM na wakazi wa Lindi, katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana, wakati akitangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba.
Mwimbaji nyota wa miondoko ya Taarab, Mzee Yusuf akitumbuiza katika mkutano huo.
Mwanasiasa mkongwe nchini, Sir. George Kahama akizungumza na wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana, wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (wa tatu kushoto waliokaa), alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba, katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana. Wengeni (kutoka kushoto) ni Katibu wa CCM Mkoa wa Lindi, Adelina Gefi na Mke wa Waziri Membe, mama Dorcas Membe.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto), akimpongeza Mwanasiasa mkongwe nchini, Sir. George Kahama baada ya Mzee Kahama kuhutubia umati wa  wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa.
Mama Dorcas Membe mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe, akimpongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi, Mzee Ali Mtopa baada ya kuhutubia umati wa  wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoani humo jana, wakati Mheshimiwa Membe (katikati), alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba.

No comments: