Tangazo

June 7, 2015

GULIO LA AIRTEL SMARTPHONE BAZAAR LAPATA MAFANIKIO MLIMANI CITY DAR

Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio Kaniki, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana  na Gulio la Airtel na Huawei Smartphone  lililofanyika Mlimani City wikiendi hii. Gulio linalomuwezesha mteja kujishindia zawadi mbali mbali pale anaponunua simu ya Huawei.Gulio hili lilianza Ijumaa, Jumamosi na Jumapili na litaendelea wiki ijayo siku ya Ijumaa, Jumamosi na Jumapili pale Kibo Complex Tegeta.
Baadhi ya Wateja waliofika katika Gulio hilo.
Meneja Masoko wa Huawei, Bi Lydia Wangari (kushoto) na Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki wakionyesha baadhi ya simu zinazouzwa katika Gulio la Airtel na Huawei Smartphone. Gulio hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki hii pale Mlimani City na kuwawezesha Wateja kupata ofa mbalimbali pale unaponunua simu hizo.

No comments: