Tangazo

April 30, 2018

Usalama Mahala pa Kazi, TANESCO yaibuka Kidedea yakabidhiwa Ngao, IRINGA

 
Shirika la Umeme TANESCO, limeibuka Kidedea Kwa Kupata Ushindi Kwenye Shindano la Usalama Mahali pa Kazi lililoendeshwa na Taasisi ya OSHA katika Viwanja vya Kichangani Manispaa ya IRINGA.

TANESCO imepata Ushindi huo Kupitia Sekta ya Huduma, ambapo imekabidhiwa Ngao na Cheti ikiwa ni Heshima ya Kutambuliwa Kama Taasisi ambayo imefanya Vizuri Kwa Kuzingatia Usalama Mahala pa Kazi.

Baada ya Shirika hilo la Umeme Kutangazwa Mshindi na Kukabidhiwa Ngao, Afisa Afya na Usalama Makao makuu NELSON MNYANYI amesema Elimu ya Afya na Usalama imekuwa Kichocheo Kikubwa katika Kupunguza Ajali kwa Wafanyakazi wa TANESCO pamoja na Wananchi kwa Ujumla.

Kwa Upande wake Afisa Afya na Usalama FRED KAYEGA akielezea Ushindi huo amesema licha ya Kupokelewa kwa Faraja, ni Motisha kwa TANESCO kuendelea Kufanya Vizuri zaidi Kwenye Sekta ya huduma Kwa Kuzingatia Usalama Mahala pa Kazi.

Katika Banda la TANESCO elimu mbalimbali kuhusu Afya na Usalama na Elimu Kuhusu Matumizi Bora na Sahihi ya Umeme iliweza Kutolewa kwenye Viwanja vya Kichangani Manispaa ya Iringa.
Waziri wa Viwanda, Biashara ya Uwekezaji CHARLES MWIJAGE akiangalia Baada la TANESCO mara Baada ya Kulitembelea Katika Viwanja vya Kichangani Manispaa ya Iringa, ambapo Shirika hilo limeibuka Mshindi Kwenye Sekta ya Huduma Kupitia Mashindano ya Usalama Mahala pa Kazi yaliyoendeshwa na Taasisi ya OSHA.
Maaofisa wa Shirika la Umeme TANESCO, Kutoka Kushoto Sylvester Matiki ( Afisa Masoko ), Nelson Mnyanyi ( Afisa Usalama ), Fred Kayenga ( Afisa Muandamizi Usalama na Afya Mahali pa kazi ) pamoja na Hassan Athumani (Mwenyekiti wa majadiliano TUICO TANESCO) wakifurahia Ushindi wa Ngao na Cheti Baada ya Kukabidhiwa Kama Washindi Kwenye Sekta ya Huduma Kupitia Mashindano yaliyoendeshwa na Taasisi ya OSHA katika Viwanja vya Kichangani Manispaa ya Iringa.
Wananchi Mbalimbali Katika Manispaa ya Iringa Waliofika Katika Banda la TANESCO katika Viwanja vya Kichangani Wakipewa Elimu Kuhusu Afya na Usalama pamoja na Matumizi Bora na Sahihi ya Umeme.
Afisa wa TANESCO, Kitengo cha Huduma kwa Wateja ENIDY ELSON akitoa Elimu ya matumizi Bora ya Umeme kwa Wanafunzi na Wananchi Waliofika Kwenye Banda la Shirika hilo Wakati wa Shindao la Usalama Mahala pa Kazi lilioendeshwa na Taasisi ya OSHA katika Viwanja vya Kichangani Manispaa ya Iringa.

No comments: