Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), George Mulamula (wa tatu kulia), akikabidhi cheti kwa Mwalimu wa Hisabati na Sayansi wa Shule ya Msingi Kijitonyama, Wilfred Ringo. xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Airtel kuanzisha Maabara ya Kompyuta kwa ajili ya wanafunzi na vijana kujifunza na kuvumbua application mbalimbali
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikian na DTBi wametoa mafunzo kwa walimu wa shule za msingi na sekondari ikiwa ni katika matayarisho yakufungua maabara ya kompyuta yanayotegemea kuzinduliwa mwezi huu.
Mafunzo hayo yametolewa na walimu 6 toka katika Kituo cha Elimu cha Galway nchini Ireland kwa lengo la kuwapatia uwezo , mbinu na maarifa ya technoologia ya kompyuta ili kuweza kuwafundisha wanafunzi watakaojiunga na kutembelea maabara hiyo ujuzi utakaowawezeshaa kutengeneza program ndogo ndogo na baadaye kuweza kuvumbua program kubwa zenye kuleta suluhisho kwa mahitaji mbalimbali ya biashara na jamii.
Maabara ya Airtel Fursa itatatoa fursa kwa vijana wenye malengo ya kujifunza masomo ya Tehama kuongeza ujuzi, na kutoa mwanga kwa vijana kuwa wabunifu kwa kuzindua application mbalimbali ambazo zitaweza kuwaingizia kipato.
Akiongea wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) chini ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), George Mulamula“ alisema kutokana na changamoto iliyopo kwa sasa ya wanafunzi wengi kutumia kompyuta kwa mara ya kwanza wanapoingia katika elimu ya chuo kikuu kumefanya kuwe na ufinyu katika ubunifu na kutumia technologia katika ujasiriamali. Tunaamini maabara ya Airtel Fursa yatatoa mwaya kwa vijana kujifunza masomo na kuvumbua mambo mengi wakiwa katika umri mdogo.
Mafunzo haya kwa walimu tunayotoa leo ni uthibitisho wa dhamira yetu katika kuhakikisha tunakuwa na walimu bora watakaowasaidia wanafunzi kujikita kwenye technologia na kuwa wabunifu. Aliongeza Mulamula
Kwa upande wake Meneja huduma kwa jamii wa Airtel, Bi Hawa Bayumi alisema “ tumejipanga kuwawezesha vijana kuzifikia ndoto zao kwa kuanzisha maabara hii yenye kompyuta za kujifunzia na kuwawezesha wanafunzi kujifunza mafunzo mbalimbali yatakayowawezesha kutanua wigo wao”
kupitia program ya Airtel Fursa tunayo application ya VSOMO iliyotengenezwa na kjana wakitanzania ambao leo hii inawawezesha maelfu ya watanzania kuipakuwa na kusoma masomo ya ufundi ya VETA kupitia simu zao za mkononi. Tunaamini maabara hii itakuvumbua na kukuza zipaji vingi na kuleta uvumbuzi katika Tehama. Aliongeza Bayumi.
|
No comments:
Post a Comment