Afisa Uhusiano na
Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kulia) akikabidhi zawadi ya kitita cha
shilingi milioni 6, kwa mshindi wa droo ya tatu ya promosheni ya Airtel
"Jiongeze na Mshiko", Agricius Kapinda katika hafla iliyofanyika
jijini Dar es Salaam jana. Anayeshuhudia (katikati) ni Afisa Huduma za Ziada wa
Airtel, Fabian Felician.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
•Washindi wazawadiwa pesa taslim.
·Zaidi ya milioni 90 bado kushindaniwa
Dar es Salaam
Airtel Tanzania imetanga washindi wa droo yake ya nne ya
promosheni ya "Jiongeze
na Mshiko" katika ofisi za makao makuu ya Airtel zilipo Morocco
jijini Dar Es Salaam, ambapo wateja wanaweza kushinda zawadi ya fedha kila wiki
ya shilingi tatu , milioni moja na mwisho wa promosheni mteja ataweza
kuondoka na kitita cha shilingi milioni 50.
Akiongea
wakati wa droo hiyo ,Afisa uhusiano na matukio wa Airtel Dangio
Kaniki alisema leo tunatangaza washindi wawili wa promosheni ya"Jiongeze
na Mshiko" ambapo
watajishindia pesa taslim shilling milioni tatu na milioni moja kila mmoja. Ninayo
furaha kutangaza washindi hao ambao ni Josephat Mahinda(25) Askari
Magereza wa wa Mkoa wa Manyara yeye amejishindi shilingi milioni 3 , na
mshindi wa pili ni Daudi Ally Kingonji (31) mfanya biashara na mkazi wa
Kiwalani Dar Es Salaam yeye amejishindi shilingi milioni 1.”
Kaniki
aliongeza kwa kusema, mpaka sasa Airtel imeshakabidhi zawadi kwa washindi mbali
mbali hapa nchini. Na leo hii tumewakabidhi washindi wa droo ya tatu
ambao ni Shangai Rodger (53) mkazi wa Tanga yeye amejishindi shilingi milioni 3 , na
mshindi wa pili ni Afrillious Kapinaa (21) mwanafunzi na mkazi wa mkoa wa Dar Es Salaam yeye
amejishindi shilingi milioni 1 waliopokea zawadi zao leo hii asubuhi.
Akiongea
na waandishi wa habari Afrillious Kapinaa mwenye umri wa miaka 12, aliishukuru
Airtel kwa kuanzisha promsheni hii. Ushindi wake ulikuja kama bahati na msaada
mkubwa sana katika maisha yake ya uanafunzi. “Wazazi wangu wako Songea, ushindi
huu wa milioni moja utanisaidia kutimiza mahitaji yangu nikiwa hapa
chuoni. Nawahimiza Wateja wengine wa Airtel kujiunga na prmosheni hii kwani ya
ukweli kabisa”.
"Tunawashukuru
wateja wetu na watanzania wote walioshiriki mpaka sasa katika promosheni hii.
"Tunaamini ushindi huu utawawezesha wateja wetu kupata fedha za kuendesha
shughuli zao za kiuchumi na kuboresha maisha yao, hilo ndilo lenge letu kama
Airtel. Natoa wito kwa watanzania kujiunga na kushiriki bure kwa kutuma
ujumbe wenye neno BURE kwenda namba 15470 na kupata nafasi ya kushindia kupitia
droo zetu za kila wiki." alimalizia Kaniki.
No comments:
Post a Comment