Meneja wa Huduma kwa Jamii wa Airtel, Hawa Bayumi (wa
tatu kushoto), akikabidhi Ng’ombe wa maziwa kwa kijana Jonathan Tarimo, ikiwa
ni sehemu ya msaada wa Ng’ombe wawili wa maziwa na zizi jipya, alivyomkabidhi
kupitia mpango wa Airtel ‘Fursa Tunakuwezesha’, katika Kijiji cha Migungani ‘B’
wilayani Monduli mkoa wa Arusha jana. Wanaoshuhudia (kutoka kushoto) ni Baba
mzazi wa kijana huyo, Clemence Tarimo na Mratibu wa Masoko wa Airtel wilaya ya
Monduli, Polas Emmanuel.
XXXXXXXXXXX
AIRTEL Tanzania kwa kupitia mpango wake wa Airtel Fursa “Tunakuwezesha” imemkabidhi kijana Jonathan Clement
mkazi Migungani kata ya Mto wa Mbu wilaya ya Monduli mkoani
Arusha ng’ombe wawili, banda la kisasa pamoja na mafunzo ya
biashara ambayo itamsaidia kuinua biashara yake ya ufugaji na
kumuongezea kipato chake.
Jonathan kijana mwenye umri wa miaka 21 na elimu ya
kidato cha nne amekabidhiwa mtaji huo ambapo awali alikuwa na ngomb’e
wawili na banda lililochoka na alikuwa na changamoto ya elimu
ya ufugaji na madawa ya mifugo.
Jonathan ameishukuru kampuni ya simu za
mikononi ya Airtel kwa kumpatia msaada huo amesema “biashara yangu ya
ufugaji sasa itapiga hatua. Naamini miaka michache ijayo nitakuwa na mifugo
mingi sana na soko langu la maziwa litakuwa kwa kasi. Na vile vile itaniwezesha
kuinua familia na biashara yangu kwa ujumla”.
“Hii ni bahati ya peke kwangu kutoka
Airtel, kwani ni vijana wengi sana wanatamani kupata hivi nilivyovipata lakini
hawakupata bahati hii. Nawahimiza vijana wengine wasikate tamaa na
wajitokeze kwa wingi kwani Airtel Fursa ipo kutuwezesha vijana”.
Akizungumza baada ya makabidhiano,
Meneja huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi, alisema “mpango huu
ulibuniwa ili kuwawezesha vijana na kuwakwamua kiuchumi. Jonathan amepitia
changamoto nyingi kufikia hapa alipo alianza na ngombe wa kukopeshwa kutoka kwa
mjomba wake kwa makubaliano kwamba atakapopata ndama wa kwanza atakuwa wa
kwake. Lakini leo hii tumemuwezesha kuwa na jumla ya ng’ombe watatu kwenye zizi
lake”.
“Airtel kupitia mradi wake wa Airtel
Fursa “Tunakuwezesha” imempatia msaada huu Jonathan baada yakuridhishwa na
hatua ya ufugaji pamoja na kuonyesha nia yakuwa mfugaji bora hapa nchini”
alisema.
Bayumi aliwataka vijana wachangamkie fursa hiyo na kuongeza kuwa mpango
huu unawalenga vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ambao watapokea misaada ya
vifaa au thamani ili kuweza kutimiza malengo yao.. “Program hii inahusisha vijana kutoka sehemu mbalimbali
nchini alisema.
Ili kijana kushiriki au kufaidika na Airtel Fursa atatakiwa kutuma ujumbe mfupi kwenda kwa namba 15626 na kuweka maelezo yafuatayo:-
Jina, Umri, aina ya biashara na eneo. Pia wanaweza kutuma maombi yao
kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com,mailto:airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara. Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com .
kwa kupitia barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com,mailto:airtelfursa@tz.airtel.com ambapo watatakiwa kutuma jina kamili, umri, na aina ya biashara. Maelezo kuhusu program ya Airtel FURSA pia yanapatikana kwenye tovuti ya Airtel www.airteltanzania.com .
No comments:
Post a Comment