Nahodha wa timu ya Moro Kids Dissy Job
akinyanyua kombe la ubingwa la Airtel Rising Stars baada ya kutawazwa
mabingwa wa mkoa wa Morogoro.
|
Timu ya Moro Kids wakipozi na kombe la ubingwa baada ya kutawazwa
mabingwa wa mkoa wa Morogoro katika mashindano ya Airtel Rising Stars.
mabingwa wa mkoa wa Morogoro katika mashindano ya Airtel Rising Stars.
xxxxxxxxxxxxxxx
Timu ya Moro Kids imeukwaa uchampioni wa mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars mkoa wa Morogoro baada ya kuwafunga Kihonda 2-1 katika mchezo wa funga dimba uliopigwa jana kwenye uwanja wa Shujaa mjini Morogoro.
Ushindi
huo kwenye mchezo wa jana uliohudhuriwa na mashabiki wengi uliwawezesha Moro
Kids kufikisha pointi sita wakifuatiwa na timu ya Tecfort iliyohitimisha
mashindano hayo ya mkoa ikiwa na pointi tatu.
Wakati
huo huo chama cha soka mkoani Morogoro (MOREFA) kimetangaza kikosi cha
wachezaji 20 kitakacho uwakilisha mkoa huo katika mashindano ya taifa
yaliyopangwa kuanza kutimua vumbia kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini
Dar es Salaam kuanzia Septamba 11 hadi 21.
Katibu
Mkuu wa MOREFA Emmanuel Kimbawala amesema kikosi hicho, kilichochaguliwa
wakati wa michuano hiyo mkoani Morogoro kimeundwa na wachezaji wenye vipaji na
kuonyedha dhamira ya dhati ya kuweza kutwaa tena ubingwa wa Airtel Rising Stars
ngazi ya taifa mwaka huu.
Lengo
la mashindano ya Airtel Rising Stars ni kuwapa fursa wachezaji chipukizi wa
soka, wasichana na wavulana, kuonyesha vipaji vyao na hatimaye kuweza kuonekana
na kuchaguliwa kuchezea timu mbalimbali.
Matunda
ya Airtel Rising Stars yanaonekana katika timu za taifa za vijana na Twiga
Stars.
Mwaka
huu mashindano ya Airtel Rising Stars yanajumuisha mikoa ya kisoka ya Ilala,
Temeke, Ilala Mbeya na Mwanza kwa timu za wasichana na wavulana huku mkoa wa
Morogoro ukishirikisha wavulana peke yake wakati Arusha ni wasichana tu.
No comments:
Post a Comment