Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel Bi Dangio
Kaniki (kushoto) na Meneja masoko wa Airtel Anethy Muga (kulia)
wakionyesha simu mpya zilizoingizwa sokoni zikiwa na ofa ya Airtel smartifonika
aina ya Mgnum Bravo Z10 wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika makao makuu ya
Airtel leo.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Dar es Salaam
Octoba 22, 2015
Airtel Tanzania leo imezindua
smartifoni mpya na yenye ubora zaidi ijulikanayo kama Magnus Bravo Z10 ambapo zinapatikata sasa hivi kwenye maduka yote ya Airtel nchini zikiwa zimeunganishwa na
ofa ya Smartifonika inayompatia mteja muda wa maongezi wa dakika 150,
150MB na SMS 150 kwa kipindi cha miezi sita.
Akiongea na waandishi wa habari
Meneja masoko wa Airtel Tanzania Aneth Muga amesema “Airtel tumekuletea Simu
mpya ya Magnus Bravo Z10 ili kukuwezesha mteja wetu
kuendelea kufurahia huduma zote za Airtel na zile huduma zote za kisasa za
smartifoni ukiwa mahali popote
“Magnus
Bravo Z10 toka Airtel
inatumia laini mbili, ina radio, kioo (screen) kubwa ili kukupa raha zaidi
kuona vyema unapokuwa unaitumia, pia imewekewa kamera zenye uwezo mkubwa mbele
na nyuma za 5mp ili kukupa taswira au picha nzuri utakazopiga karibu au mbali
ukiwa na ndugu, jamaa na marafiki” alielezea Bi Muga
“Vilevile
ili uweze kufurahia huduma zote za mitandao, Airtel tumehakikisha tayari simu hii inamitandao yote ya kijamii
kama facebook, Instagram, twitter na mingine mengi” . Alisema Bi Muga
Simu hii inapatikana sasa
katika maduka yote ya Airtel nchini kwa gharama nafuu kuliko zote ya sh.
75,000 tu.
No comments:
Post a Comment