Mkuu
wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya G4S, Alfred Elia, (katikati), akizungumza
kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 14, 2016
kuhusu ushirikiano baina ya kampuni yake na taasisi ya kujitolea ya Uingereza
ya Bhubesi Pride Foundation, (BPF), ambapo taasisi hiyo inaendesha mafunzo ya
kuunyanyua mchezo wa Raga (Rugby), pamoja na kusaidia jamii pamoja na maendeleo mashuleni na
kwenye vituo vya kijamii. Shule sita sita za jijini Dar es Salaam zitashindana
katika mchezo huo Jumamosi hii jijini. Wengine pichani, ni Meneja mradi wa BPF,
Mark Cole, (kulia) na Mkuu wa masuala ya fedha wa G4S, Paul Fullers.Mkutano huo
na waandishi wa habari ulifanyika jana Machi 14, 2016 (Picha K-VIS
EMDIA/Khalfan Said)
NA K-VIS MEDIA/Khalfan
Said
TAASISI ya kujitolea ya Uingereza ya Bhubesi Pride Foundation (BPF) kwa kushirikiana na kampuni ya
ulinzi ya G4S ya jijini Dar es Salaam, inaendesha mpango wa kuunyanyua na
kuuendeleza mchezo wa Raga, (Rugby), kusaidia jamii pamoja na maendeleo
mashuleni na kwenye vituo vya kijamii.
Akizungumza kwenye
mkutano na waandishi wa habari makao makuu ya G4S barabara ya Ali Hassan Mwinyi
jijini Dar es Salaam leo Machi 14, 2016, Mkuu wa kitengo cha Mauzo na Masoko
cha G4S, Alfred Elia, amesema, tayari mafunzo hayo yamefanyika jijini Arusha na
sasa yako hapa jijini Dar es Salaam na yameanza rasminleo Jumatatu Machi 14,
2016 ambapo jumla ya shule sita za msingi ziko kwenye mpango huo.
Amezitaja shule hizo
kuwa ni pamoja na shule ya msingi, Mapambano, Makumbusho, Hananasifu, Victoria,
Mugabe na Shekilango.
Kwa upande wake, Meneja
wa BPF, Mark Cole, alisema, mpango huo unaendeshwa kwenye nchi mbalimbai za
Afrika na ni wa mwaka mmoja. “Tayari tumefanya mafunzo haya nchini Uganda,
Kenya, Tanzania, Msumbiji, Malawi, Zambia, Botswana, Namibia na Afrika Kusini,
alisema Cole
Alisema, nia ya mpango
huo ni kuunganisha jamii kupitia raga, kuelimisha thamani na stadi za maisha, pamoja
na kunyanyua uwezo wa walimu nchini, kulea viongozi wa jamii, wake kwa waume
pamoja na kuweka uwezeshaji huu kuwa endelevu.
Maendeleo ya matokeo ya
muda mrefu kupitia miradi inayoonekana, mfano kupanda miti, kwa kushirikiana na
wabia wetu katika nchi tajwa.
Tayari shirika hili kwa
kushirikiana na G4S Tanzania limeishafanya haya Arusha na Moshi ambapo watoto
zaidi ya watoto 600 wa mikoa hio walipata mafunzo ya raga pamoja na stadi za
maisha ambapo pia G4S ilipanda miti katika maeneno mbalimbali
Naye Mkuu wa masuala ya
fedha wa G4S, Paul Fullers, alisema, G4S kwa kutambua masuala ya usalama, ndio
maana imeamua kushirikiana na BPF ili kujenga uelewa miongoni mwa wanafunzi
kuhusu masuala ya usalama wawapo shuleni, mabarabarani na hata nyumbani.
“Mafundisho haya
yanafanyika kila mwaka kuanzia mwezi January mpaka Julai, ambapo shuguli za
kijamii hufanyika sambamba na makampuni yanayojitolea kudhamini- G4S Africa, akiwa
ni mdhamini mkuu na muhimu kwa hii taasisi.” Alifafanua Fullers.
Mashirika yasiyo ya
kiserikali (NGOs). Vyama vya raga kitaifa, idara mbalimbali za kiserikali,
shule za kimataifa pamoja na makampuni mbalimbali kwenye jamii husika,
kuongezea thamani katika huu uhusiano pamoja na kujengea uwezo, alisema.
Mark Cole, Meneja mradi wa BPF
Finn Sims, Meneja anayehusika na vyombo vya habari wa BPF
Paul Fullers, Mkuu wa masuala ya fedha wa G4S
Mkutano na wahanhabari ukiendelea
Wanahabari wakisikiliza kilichokuwa kikizungumzwa
Alfred Elia, akiwatambulisha wageni wake
No comments:
Post a Comment