Tangazo

June 16, 2016

Airtel FURSA yawafikia watoto 500 msimu wa Ramadhan

  • Vijana wa Airtel FURSA kujitolea kazi zao
DAR ES SALAAM
Kampuni ya za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa huduma kwa jamii  chini ya mradi wa Airtel FURSA imeanza kutoa futari  katika kindi hichi cha Ramadhan kwa vituo vinavyolea watoto waliopo katika mazingira magumu nchini.
Airtel ikishirikiana na vijana wajasiriamali wa Airtel FURSA imetoa msaada wa vyakula vitakavyowasaidia watoto walio katika vituo mbalimbali nchini kufuturu wakati wote wa msimu huu wa ramadhani.
Akiongelea kuhusu “FUTARI na Airtel FURSA” Bi Dangio Kaniki, Afisa Mahusiano na Matukio wa Airtel Tanzania alisema, “Tumeweza  kuwafikia watoto walio katika vituo mbalimbali nchini, kama sehemu ya shughuli zetu za jamii. Leo tunatoa Tshs million 10 kwa ajili  ya watoto zaidi ya 500 katika mikoa ya Mbeya, Arusha, Mwanza, Zanzibar, Dodoma na Dar es saalam.  
“FUTARI na Airtel FURSA” kwa mwaka huu imeshirikisha vijana walio nufaika na Airtel FURSA kwa kutoa sehemu ya kazi zao kusaidia jamii.Kwa namna ya pekee tunawapongeza Vijana walionufaika na Airtel FURSA Kwa kutambua changamoto nyingi zinazozikumba jamii na kushiriki kutoa kidogo walichonacho. 

Lengo la Airtel kupitia Airtel FURSA ni kuhakikisha tunagusa mahitaji ya jamii kwa ujumla, husasani watoto kupitia vituo vinavyowatunza huku tukihakikisha tunarudisha faida tunayoipata kwa kuwafikia watanzania wengi kupitia shughuli zetu za huduma za kwa jamii kwa kila mwaka.


Vituo hivyo vitakavyopata msaada kutoka Airtel  ni pamoja na  Sarnaa Islamic Ophanage center Mwanza, Kiboa Islamic Center Arusha, Nuru Ophanage Center na Hope for the future Mbeya, Swadiq Development Foundation Dodoma, Maua Daftari Zanzibar na vituo vingene vitatu  kutoka katika wilaya ya Temeke, Ilala na Kinondoni  jijiji Dar es Saalam

No comments: