Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF limefanya
semina na kuzindua mpango wa kuwaandikisha maadereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma,
Mpango huo ulifanywa kwa ushirikiano wa Manispaa ya Mji wa Dodoma, VETA ,
Trafiki Mkoa na NSSF umezinduliwa na Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu
Kazi, Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama.
Pamoja na Uzinduzi wa Uandikishaji Waziri Jenista Mhagama
aliwapatia Vifaa vya Usalama Madereva hao wa BodaBoda Mkoani Dodoma vifaa hivyo
ni Kofia ya Usalama na Kikoti Maalumu cha Usalama ambavyo vimeandikwa Namba
kulingana na Kituo cha Bodaboda Wanachofanyia Kazi. Pia Waziri amezindua mfumo
wa kuvipa namba na kuviweka alama Vibao vituo vyote vya Bodaboda mkoani Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Godius Kahyarara akiongea
na Madereva wa Bodaboda (hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa rasmi wa Kampeni ya
Kuandikisha Madereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma.
Waziri wa Nchi , Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira,Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Mpango wa kuwaandikisha madereva wa Bodaboda Mkoani Dodoma.
Meneja wa NSSF Mkoa wa Dodoma Rehema Chuma akitoa elimu
kwa Madereva wa Bodaboda wa Mkoa wa Dodoma waliouzulia zoezi la uzinduzi wa
kampeni rasmi ya kuwatambua na kuwaandikisha NSSF madereva wa Bodaboda.
Waziri akikabidhi moja ya pikipiki ambazo wamekopeshwa madereva wa Bodaboda Dodoma na Manispaa ya Dodoma. Wakishuhudia ni Mwakilishi wa Kamanda wa Trafiiki Mkoa, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF na Mkuu wa Chuo cha VETA Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akimvalisha mmoja wa Madereva wa Bodaboda Kofia Ngumu ya Usalama iliyotolewa na NSSF. Anayeshuhudia kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof, Godius Kahyarara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akimvesha Jaketi maalumu la Usalama Dereva wa Bodaboda Mkoa Dodoma akimsaidia Waziri ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Francis Mwonga.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana
na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama akikabidhi mfano wa Kituo Cha Bodaboda
kwa Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoani Dodoma Bang'ara Lucas Kang'alo akishuhudia
katikati Mkurugenzi wa NSSF Prof Godius Kahyarara.
Mwenyekiti wa Bodaboda Mkoa wa Dodoma akiwa kwenye picha
ya pamoja na Waziri wa Nchi Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Jenista Mhagama,
Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya wa Bahi Francis
Mwonga( Wa Kwanza kulia kwa Waziri), Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof Godius
Kahyarara (Kushoto kwa Waziri) na Mkuu wa Chuo cha Veta Dodoma Bw. Mattaka
baada ya kupokea mfano wa kadi ya Mwanachama ya NSSF akiwa mmoja ya wanachama
wapya waliojiunga NSSF.
No comments:
Post a Comment