Mkuu wa Idara ya Ujirani Mwema wa Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale,Mhifadhi ,Romanus Mkonda akizungumza na kina mama wanaofanya kazi ya kuponda mawe mwambao mwa ziwa Tanganyika kwa lengo la kupata kokoto ambazo TANAPA imekua ikinunua kwao kwa ajili ya ujenzi wa mioundo mbinu.
Kina mama katika kijiji cha Buhingu wilayni Uvinza mkoani Katavi wakipasua Mawe kwa ajili ya kuponda ili kupata Kokoto ambazo zimekua zikinunuliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mahusiano na Hifadhi ya Taifa ya Mahale inayopakana na kijiji hicho.
Katibu wa waponda Kokoto katika kijiji cha Buhingu Neema Jackson akisoma risala mbele ya viongozi wa Hifadhi Taifa ya Milima ya Mahale na TANAPA walioongozana na wanahabri kutembelea kina mama hao.
Kazi ya upasuaji wa Mawe katika kijiji vcha Buhingu kimekuwa pia kikifanywa na kina mama ambao umri wao umeenda ili kusaidia familia zao.
Sehemu ya kokoto zilizokwisha patikana ambazo hata hivyo kina mama hao wamelalamikia bei ndogo wanayolipa Makandarasi wanao pata zabuni ya ujenzi wa miundo mbinu ambapo wamekua wakilipwa sh 500 kwa ndoo tofauti na bei ya Sh 1000 kwa ndoo inayo lipwa na TANAPA pindi inapohitaji malighafi hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza na kina mama hao mara baada ya kusilikiliza changamoto za kina mama hao.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini (TANAPA) Pascal Shelutete akimueleza jambo na Katibu wa waponda kokoto Neema Jackson akitizama namna ya kushauri makandarasi wanaopewa dhabuni ya ujenzi na TANAPA kuhakikisha wanatumia malighafi za kina mama hao.
Menea Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pscal Shelutete akikabidhi kiasi cha Sh 100000 kwa katibu wa kina mama hao mara baada ya kusikiliza changamoto zinazowakabili.
Baadhi ya Watoto wanaoshiriki kusaidia wazazi wao katika shughuli ya upondaji kokoto katika kijiji hicho.
Kina mama wanao ponda kokoto wakifurahia na Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascla Sheluetete mara baada ya kutoa fedha kwa kina mama hao.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kigoma.
No comments:
Post a Comment