Tangazo

July 21, 2016

WANANCHI WATATU WAJIZOLEA MIFUKO 1,200 YA TWIGA CEMENT

Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Tanzania Portland Cement Ltd, Simon Delens akiponyesha kompyuta kumpata aliyeibuka mshindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya “Jijenge na Saruji ya Twiga” iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana, ambapo Mkazi wa Dodoma, Robert Kassim aliibuka mshindi na kujinyakulia mifuko 600 ya saruji. Wa pili ni Charles Chale wa Dar es Salaam aliyejipatia mfuko 400 na  wa tatu ni Athanas Nyagalu wa Dodoma mifuko 200. Kushoto walioketi ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Bakary Maggid,  Mwakilishi wa Bongo Live, Amelye Chatila (katikati). Mkuu wa Idara ya Promosheni Martha Haule. PICHA ZOTE: JOHN BADI
Mkuu wa Idara ya Promosheni wa kampuni ya Tanzania Portland Cement Ltd, Martha Haule akiwasiliana na Mkazi wa Dodoma, Robert Kassim aliyeibuka mshindi wa droo hiyo. Kushoto ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Bakary Maggid na  Mwakilishi wa Bongo Live, Amelye Chatila.
XXXXXXXXXXXXXX

DAR ES SALAAM

Washindi  watatu wa mwanzo wa promosheni ya Jenga na Twiga Cement wamepatikana leo asubuhi kwenye droo iliyochezesha  jijini Dar es Salaam.

Mshindi wa kwanza ni  Robert Kassin (39)  kazi yake ni fundi ujenzi ndiye aliyeng’ara kwenye droo ya kwanza ya Jenga na Twiga Cement  huku akipata zawadi ya mifuko 600 ya Twiga Cement Extra.

Mshindi wa pili ni Charles Chale mwanafuzi wa Chuo Cha Uhasibu , Mkazi wa Jijini Dar es Salaam amepata zawadi ya mifuko 400 ya Twiga Extra Cement na nafasi tatu ilikwenda kwa Athanas Nyagalu ambaye pia ni fundi ujenzi  mkaazi wa Chalinze Mkoani Dodoma  amepata zawadi ya mifuko 200 ya Twiga Cement Extra  Na yeye ni fundi ujenzi.

Washindi hao walipatana kwenye droo iliyochezeshwa mbele ya waandishi wa habari  na kusimamiwa na Ofisa wa Bodi ya Bahati Nasibu  Bakari  na kuchezeshwa na Kampuni ya Bongolive Amelya  Chatila.

Akizungumza kabla ya kupatikana kwa washindi hao  kwenye ukumbi uliopo ndani ya Kiwanda cha Wazo Hill Jijini Dar es Salaam kinachofahamika  kwa  jina la Tanzania Portland Cement Company Ltd (TPCC),  Mkurugenzi wa Masoko  Simon Delens alisema promosheni hiyo inafanyika kwa  kwa mara ya kwanza na  amefurahi kuona kwamba zaidi ya wateja 4,000 wameitikia na kushiriki kwa kutuma kuponi  za droo hiyo.

Promosheni hiyo ilizinduliwa inayofahamika kwa jina la ‘Jijenge Na Twiga Cement’ itadumu kwa majuma nne ilizinduliwa Julai 18 mwaka huu na kilele chake itakuwa Agosti 28 mwaka huu.

Delens alisema “Twiga Cement inajivunia kuzindua promosheni  hii  ya  kipekee ambayo  inawahusu wateja wote wa TPCC kwa kupitia promosheni hii  ya ‘Jijenge na Twiga Cement’  washindi watapata  nafasi ya  kushinda  mifuko 600 ya cement, Kampuni imetenga  jumla ya mifuko 4,800 ya cement  kwa ajili  ya promosheni hii”.

Delens aliongeza kwa kusema kuwa  Kampuni yao imeamua  kuwazawadia  wateja wake  waaminifu hivyo ametoa wito waichangamkie fursa hiyo muhimu huku akizitaja zawadi zingine zitakazokuwa zikitolewa kwenye promosheni hiyo kuwa ni  mashine  za kufyatulia matofali, mixers, matoroli, fulana  na kofia.

Delens aliongeza kwa kusema kuwa Kampuni  ya Twiga Cement ndiyo inayoongoza kwenye soko la cement nchini alimalizia  kwa kuwakumbusha na kuwahamasisha wateja  wa Twiga Cement waendelee kununua cement   wanayoitengeneza kwani endapo mteja akipata zawadi ya mifuko itamsaidia kujenga nyumba.


Akifafanua namna ya kushiri Delens alisema mara baada ya mteja kununua mfuko wake wa Twiga Extra anaona  namna maalumu  ya siri itakayokuwa imewekwa kwenye  valvu  ya kila mfuko  wa Twiga na kutakiwa kuituma namba hiyo ya siri kwenda namba 0789 000 666 ambapo atakuwa ameingia moja kwa moja kwenye droo ya wiki  washindi watakuwa wakipatikana  kila  wiki.

No comments: