Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akitembelea kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu
Hassan akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba Mhandisi.Leonce namna gesi inavyopokelewa na kuchakatwa na kusafirishwa kwa watumiaji
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu
Hassan akiangalia mfumo wa uendeshaji na usalama wa kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu
Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa kiwanda cha kuchakata gesi cha Madimba mkoani Mtwara.
.......................................................................
Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka wafanyakazi wa kiwanda cha kuchakata gesi asilia kilichopo
Madimba mkoani Mtwara wawe wazalendo na wafanye kazi kwa bidii katika kulinda
na kuutunza uwekezaji huo mkubwa ambao serikali inautegemea katika uzalishaji
wa nishati ya umeme wakati taifa linaelekea kwenye nchi ya viwanda.
Makamu wa Rais ametoa kauli
hiyo wakati akizungumza na wafanyakazi na watendaji wa kiwanda hicho baada ya
kutembelea kiwanda kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo kwa lengo la
kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa kiwandani hapo akiwa katika ziara
yake ya kikazi ya siku nne mkoani Mtwara.
Amesema kiwanda cha
kuchakata gesi asilia ni hazina kubwa kwa
Taifa hivyo ni kikalindwa na kutunzwa ipasavyo kutokana na umuhimu wake katika
uzalishaji wa nishati ya umeme kwa maendeleo ya nchi.
Makamu wa Rais pia amewashukuru
na kuwapongeza wafanyakazi wa kiwanda hicho cha kuchakata gesi asilia cha
Madimba na amewahakikishia kuwa serikali itaendelea kuwajali na kuwathamini
katika utendaji wao wa kazi na kwamba serikali itahakikisha wafanyakazi wa
kiwanda hicho wanapewa motisha ya kutosha ili waongeze maradufu utendaji wao wa
kazi ili malengo ya serikali ya kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia viwanda
inatimia kwa sababu taifa litakuwa na nishati ya umeme ya uhakika.
Makamu wa Rais amewataka
watendaji wa Shirika la Maendeleo la Petroli (TPDC) ambalo linasimamia mradi
huo kuhakikisha wanatenga fedha kwa ajili ya kusaidia huduma za jamii katika
vijiji vinavyozunguka mradi huo kila mwaka ili wananchi waweze kuwa walinzi wa
mitambo hiyo.
Akitoa maelezo mafupi ya
mradi huo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe amesema
kiwanda hicho kina uwezo wa kuchakata gesi ya futi za ujazo milioni 210 kwa
siku. BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
No comments:
Post a Comment