Tangazo

October 3, 2016

GREEN WASTEPRO YAUNGANA NA MAKAMU WA RAIS, RC MAKONDA KUPANDA MITI DAR

Wafanyakazi wa Kampuni ya Usafi ya Green WastePro wakifanya usafi katika eneo la Gymkhana kabla ya kuanza shughuli ya kupanda miti.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu akiwahutubia wananchi waliojitokeza kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni ya Mti Wangu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumzia kampeni ya Mti Wangu pamoja na kumkaribisha mgeni rasmi, Makamu wa Rais, Samia Suluhu kuzungumza na wananchi waliojitokeza katika eneo la Gymkhana kwa ajili ya kupanda miti.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumzia wilaya yake imevyojipanga kupanda miti mingi ili kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda la kila mwananchi kupanda mti.

Kampuni ya usafi ya Green WastePro Ltd. imekuwa moja ya makampuni mkoani Dar es Salaam ambayo yameungana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema kufanya uzinduzi wa kampeni ya Mti Wangu ulioambatana na kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya Dar.

Kwa upande wa wafanyakazi wa Green WastePro walipanda miti katika eneo la Gymkhana lililopo pembezoni na bahari ya Hindi wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Anthony Mark na Meneja Mwendeshaji wa kampuni ya usafi ya Green WastePro Ltd, Abdallah Mbena.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu akiwapungia mkono wananchi waliojitokeza kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni ya Mti Wangu.
Mkurugenzi wa Green WastePro, Anthony Mark akikabidhiwa mti na Diwani wa Kivukoni, Henry Massaba kwa ajili ya kuanza shughuli ya kupanda mti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mti Wangu iliyo na lengo la kuhakikisha jiji la Dar linakuwa na miti mingi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Mkurugenzi wa Green WastePro, Anthony Mark akipanda mti wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mti Wangu.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akipanda mti katika eneo la Gymkhana, mbele yake ni Afisa Mazingira wa Wilaya ya Ilala, Ester Masome
Wafanyakazi wa Green WastePro wakiongozwa na Meneja Mwendeshaji wa kampuni hiyo, Abdallah Mbena wakipanda mti na Afisa Mazingira wa Wilaya ya Ilala, Ester Masome.
Wafanyakazi wa Green WastePro wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema baada ya zoezi la kupanda miti.
Wafanyakazi wa Green WasteProwakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa hospitali ya Agha Khan.
Mkurugenzi wa Green WastePro, Anthony Mark akiwa katika picha ya pamoja na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Waziri Kindamba, Meneja Mwendeshaji wa kampuni ya Green WastePro Ltd, Abdallah Mbena na watumishi wa Wilaya ya Ilala.

No comments: