Diwani wa kata ya Kata ya Mponde wilayani
Bumbuli Mkoani Tanga, Edwin Mahunda akikata utepe kuzindua mnara wa mawasiliano
uliojengwa kwa ushikiano kati ya Airtel na Mfuko wa Maendeleo wa Mawasiliano
kwa Wote (UCSAF). Anayeshuhudia (wa pili kulia) ni Meneja Mauzo wa Airtel
Tanga, John Nada. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
- Yapeleka huduma kwa
vijiji 16 kuimarisha ulinzi na mawasiliano kwa jamii mkoani humo.
TANGA
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imewafaidisha zaidi ya wakazi
elfu kumi na nne waishio katika vijiji vya Lushoto na Bumbuli kwa kuwapatia
mawasiliano ya uhakika kupitia ushirika wao na mfuko wa Maendeleo wa
mawasiliano kwa wote UCSAF yaani Universal Communication Services Fund.
Uzinduzi wa mnara wa mawasiliano wa Airtel katika kata ya Mponde
Wilayani Bumbuli Mkoani Tanga, umekuja ikiwa ni wiki moja toka Mfuko wa
maendeleo wa Mawasiliano kwa wote na Airtel walipozindua minara mingine mitatu
mkoani Dodoma.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mnara huo, Meneja Mauzo wa Airtel
Tanga, John Nada alisema "Airtel tumejipanga kuendelea kutoa
mawasiliano ya uhakika hasa kwa kipindi hiki ambacho TCRA wamezindua
huduma ya kuwawezesha wateja kuhama mtandano akiwa na namba ileile ikiwa
hawapati huduma nzuri na za uhakika, hivyo basi kwa wakazi wa Balangai, Hebangwe,
Kilimandege, Mahanga, Maluda, Mhezi, Mkinga, Mlai, Mlola, Mpalalu, Ndeme,
Nkombola, Ponde, Sakare na Sakarre Airtel ndio mtandao wenu wa
ukahika kwa sasa”
“Tunawaomba wakazi wote mtumie fursa hii ya mawasiliano kwa kuwa
wabunifu zaidi, tumumieni huduma ya Airtel Money kwa kuwa
pia mko mbali na huduma za kibenki tumeni na kupokea pesa ili kuboreshe kilimo
kwa kutumia mawasiliano haya ya uhakika toka Airtel” alisisitiza Bw, Nada.
Kauli ya wananchi juu ya tatizo la mawasiliano
zilithibitishwa na diwani wa kata hiyo ,Mh Edwin Mahunda kwamba wakazi wa Kata
hiyo walikuwa wakipanda juu ya miti na kwenye vilele vya milima wakitafuta
mawasiliano ili kufanya mawasiliano ya kibiashara na mambo mengine ya kijamii.
“Tunawashukuru sana Airtel na UCSAF kwa jitihada zao za kutuletea
mawasiliano, mawasiliano haya yatasaidia wakazi wa hapa kijijini na pia
yatawasaidia wanaishio mbali na hapa ili kuweza kufanya shughuli zao vyema,
awali hali ilikuwa mbaya sana, ilikuwa huwezi kupiga simu mpaka ufike sehemu
yenye muinuko” alieleza Mahunda.
Diwani huyo aliendelea kusema kuwa “ninawaahidi wadau wa
mawasiliano Airtel na UCSAF kwamba tutayalinda mawailiano haya na tutayatumia
vyema ili kukuza shughuli za maendeleo ya kijamii na uchumi wa Wilaya yetu ya
Bumbuli Mkoani Tanga.
Pamoja na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kimila na serikali
pia Uzindunzi wa mnara huo katika kijijii cha kata ya Mponde Wilayani Bumbuli
Mkoani Tanga ilipambwa na ngoma na burudani za asili za vijiji hivyo ambazo
huchezwa mara kwa mara wanapokuwa na jambo la furaha kwa jamii zao.
No comments:
Post a Comment