Waandishi wa habari wakishuhudia uzinduzi wa bia chapa Allsopps ambayo inauzwa katika soko la Afrika mashariki. |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa SBL na waandishi wa habari mara baada wa bia chapa Allsopps ambayo inauzwa katika soko la Afrika mashariki. |
Mwanza, Machi 8, 2017- Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella leo ameipongeza Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa kuzalisha bidhaa zenya ubora wa hali juu jambo ambo limiweizesha kampuni hiyo kushinda tuzo mbalimbali za ubora ndani na nje ya nchi.
Mongella alitoa kauli hiyo wakati alipokitembelea kiwanda cha Bia cha SBL cha Mwanza ambako pia aliipongeza kampuni kwa mchango wake katika maendeleo ya kiuchumi ya nchi kupitia uzalishaji wa ajira, ulipaji kodi na hali kadhalika programu za kusaidia jamii.
“SBL ni mdau katika ajenda ya maendeleo ya nchi yetu. Kama serikali tutajaribu kuanzisha mazingira ambayo yanawezesha biashara kama hii ili istawi vizuri na kuvutia uwekezaji pia,” alisema Mongella.
SBL inazalisha chapa za bia ambazo ni Serengeti Premium Lager, Pilsner, Tusker Lager, TuskerLite, Kibo Gold, Guinness stout, Uhuru na Kick na hali kadhalika kusambaza pombe kali zinazofahamika duniani ambazo zinazalishwa na kampuni yake uwekezaji Diageo.
Mwezi uliopita Kiwanda cha SBL cha Mwanza kilianza uzalishaji wa bia chapa Allsopps ambayo inauzwa katika soko la Afrika mashariki.
“Hatua ya kuzalisha Allsopps katika kiwanda chetu cha Mwanza ni sehemu ya mbinu ya uendeshaji kikanda ya EABL. Hili limekuwa na matokeo ya kunufaisha kwa masoko yote na kwa biashara yetu,” alisema Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John Wanyancha.
Kwa mujibu wa Wanyancha, SBL inaendesha miradi kadhaa ya kuisaidia jamii nchi nzima katika maeneo ya upatikanaji wa maji, utoaji wa elimu- ambapo wanafunzi walio na weledi mkubwa kutoka mazingira yenye uhitaji hupatiwa udhamini wa masomo kwa ajili ya kusomea kozi za shahada ya kwanza katika vyuo vikuu vya ndani na hali kadhalika kampeni ya Ukiwa Umekunywa Usiendesha gari ambayo inahamasisha unywaji wa kistaarabu.
No comments:
Post a Comment