Baadhi
ya wafanyakazi wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakifurahia wakati wa
kusherehekea siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga wilayani
Temeke jijini Dar es Salaam, Machi 8, 2018.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAFANYAKAZI
Wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, leo Machi 8, 2017, wameungana na wenzao
katika kusherehekea siku ya Wanawake Duniani kwenye viwanja vya Mwembe- Yanga
jijini Dar es Salaam.
Katika
maadhimisho hayo yaliyohanikizwa na mvua za rasharasha, wanawake hao wakiwa na
furaha, walipita mbele ya viongozi wakuu wa mkoa na kuonhyesha mabango yao
yaliyokuwa na ujumbe tofauti tofauti.
Maadhimisho
ya Siku ya Wanawake Duniani Mwaka huu yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “Tanzania
ya viwanda, Wanawake ndio Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi”.
Kauli mbiu
hiyo inalenga kuikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa kujenga mazingira wezeshi kwa
Wanawake hasa kutambua mchango wao katika kuleta Maendeleo yao na
ya jamii kwa ujumla.
Katika
maadhimisho hayo ya siku ya Wanawake Duniani Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya
ya Temeke, Felix Lyaviva, ambaye alimuwakilisha Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye awali Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
ilisema Mkuu huyo wa Mkoa ndiye angekuwa mgeni rasmi lakini hakutokea.
Katika
hotuba yake, Mkuu wa Wilaya ya Temeke, alisema jamii inapaswa kutimiza wajibu wake ikiwa ni
pamoja na kuwashirikisha, kuwaamini na kuwapa Wanawake haki sawa katika nafasi
za Elimu, Uchumi na uongozi ili wawe chachu ya mabadiliko yenye lengo la kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Baadhi ya akina mama wa taasisi ya THTU nao wakipita mbele ya jukwa kuu.
No comments:
Post a Comment