Mkuu
wa wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula (katikati) akikata utepe kuzindua
manara wa mawasiliano wa mwakashahala ulipo kijiji cha Ngukumo kata ya
Nkiniziwa Wilayani Nzega ambapo pamoja na mnaro huu Airtel imewasha minara
mingine mitatu ya mawasiliano katika kata za Kahamanhalanga , Songambele na
Itumba na kuwawezesha wakazi zaidi ya elfu 32 kupata huduma za mawasiliano
mkoani Tabora. wakishuhudia wapili kulia ni Meneja Mauzo wa Airtel
Tabora, Fidelis Lugangila akiwa pamoja na wajumbe wa serikali
ya kijiji cha Ngukumo
XXXXXXXXXXXXXXX
TABORA
WAKULIMA na
wafugaji wa kijiji cha Ngukumo kata ya Nkiniziwa wilaya ya
Nzega mkoani Tabora wameipongeza Airtel kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma za
mawasiliano ya uhakika na kuwawezesha kuangalia bei za bidhaa na kutafuta
masoko kupitia simu zao za mkononi.
Hayo yalisemwa na
wakazi wa kijiji cha Ngukumo wakati wa uzinduzi huduma za mawasiliano
utakaowawezesha wakazi zaidi ya elfu 32 kutoka katika vijiji 6 kupata
huduma za mawasiliano baada ya Airtel kuwasha minara ya mawasiliano katika
maeneo ya Mwakashahalala Kahamanhalanga,
Songambele Itumba mkoani hapo
‘’Tumekuwa tukipata changamoto nyingi sana
ikiwemo mawasiiano hafifu ambapo ilibidi kusafiri umbali mrefu kupata huduma za
mawasiliano, Tunaishukur kampuni ya Airtel kwa kuona ni vyema kutufikishia
huduma za mawasiliano hapa na kutuunganisha na ndugu jamaa na
wafanyabiashara katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi
alisema mkazi wa kata ya Nkiniziwa, John
Akiongea
wakati wa uzinduzi, Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Godfrey
Ngupula alitambua na kupongeza juhudi zinazo fanya na Airtel katika
kuhakikisha huduma za mawasiliano zinapatikana kwa wote kufatia mchango wake
muhimu katika kukuza uchumi wa nchi na kusema ni muhimu kuwa na mawasilino bora
kwani kichocheo kikubwa katika kuboresha maisha ya watanzania na kurahisisha
shughuli zao za kijamaa na kiuchumi.
“Naamini mawasialiano
haya yataweesha biashara katika wilaya hii kukua, na wakulima watanufaika na
huduma mbalimbali za simu zitakazowawezesha kutafuta masoko ya bidhaa zao, kuangalia
bei ya mazao, lakini pia watatumia huduma ya Airtel Money kwaajili ya kufanya
malipo na manunuzi kwa njia ya simu. Nawaasa wakazi wa wilaya ya Nzega kutumia
mawasiliano haya vyema na kuboresha maisha yao” aliongeza Ngupula
Kwa upande wake
Meneja wa Airtel mkoa wa Tabora, Phidelis Lugangila alisema “Airtel
imejipanga kutoa huduma bora na za uhakika na kuwaomba wakazi wa kijiji cha
Ngukumo na vijiji vya jirani kutumia huduma na bidhaa za Airtel kupata
kipato kupitia huduma zetu kama vile Airtel Money kwa kuwa mawakala
na kupata kamisheni kila mwezi na vilevile kutengeneza ajira kwa vijana wengi.
Wakazi wa mwashala
wanajishughulisha zaidi na kilimo cha mahindi, pamba, Karanga na Mpunga pamoja
na ufugaji.
No comments:
Post a Comment