Mkurugenzi
wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Beatrice Singano na Mkurugenzi Mtendaji
wa Maendeleo Bank Ibrahim Mwangalaba wakisaini makubalianao
ya uzinduzi wa huduma ya Timiza Vikoba kwa ajili ya
kutoka mikopo kwa vikundi vidogo bila dhamana.
xxxxxx
· - Airtel Money na Maendeleo Benki
kuviwezesha Vikundi vya Vikoba nchini
- Vikundi vya vikoba kupata njia ya kisasa
na salama zaidi ya kuendesha shughuli zao za kifedha
Dar
es Salaam, Jumanne 4, Aprili 2017, Airtel Tanzania kwa kushirikiana na
benkiya Maendeleo leo wamezindua huduma mpya ijulikanayo kamaTimizaVikoba yenye
lengo la kuviwezesha vikundi vya vikoba nchini kutumia njia ya kisasa na salama
itakayorahisisha ukusanyaji wa michango, kutoa mikopo na marejesho ya mikopo
kwa urahisi kabisa.
Huduma
hii yaTimiza Vikoba inawawezesha
wateja wa Airtel walio katika vikundi vya kuanzia watu 5 hadi 50 kupata huduma
za kifedha masaa 24 siku saba za wiki kwa gharama nafuu kwa kupiga
*150*60# na kisha kuingia kwenye menu ya Airtel
Money na kusajili kikundi na
kufungua akaunti ili kufaidika na huduma ya kutuma michango yao ya kila wiki,
kuomba mikopo na kufanya marejesho ya mikopo wakiwa nyumbani au mahali popote
pale kwa usalama na urahisi zaidi.
Akiongea
wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel , Bi
Beatrice Singano Mallya alisema” huduma ya Airtel Money imekuwa ikiongoza kwa
huduma za kibunifu na kisasa zaidi na leo hii tunazindua ushirikiano wa kipekee
na benki ya Maendeleo kupitia huduma ya Airtel Money ili kuwawezesha
wafanyabishara katika vikundi vya Vikoba nchi nzima kufanya miamala yao ya
kifedha kwa njia salama, uhakika na urahisi zaidi.
Huduma
hii italeta uwazi na kuwawezesha vikundi vya vikoba kuhakiki taarifa zao kwa
kupata taarifa za miamala mbalimbali kwa wakati kupitia simu zao za
mikononi. Tunaamini huduma hii itachochea wafanyabiashara bila kujali
maeneo walioko kujiunga na kutengeneza vikundi vya vikoba ili kunufaikana
kukuza biashara zao
Timiza
Vikoba ni udhibitisho wa dhamira yetu ya kutoa huduma za kibunifu zinazoendana
na mahitaji ya wateja wetu hasa kuleta unafuu na urahisi kupitia huduma yetu ya
kifedha aliongeza Bi Singano.
Kwa
upande wake , Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank ,Ndugu Ibrahim Mwangalaba
alisema “ Maendeleo benki ni benki inayokuwa kwa kasi nchini kwa kutoa
huduma mbalimbali zenye gharama nafuu,zenye uraisi wa kutumia ikiwemo ile ya
akaunti za kuweka akiba , kutoa mikopo na huduma nyingine nyingi.
Maendeleo
benki leo tunajisikia fahari kushirikiana na Airtel katika kuleta huduma
yaTimizaVikoba, huduma hii itasaidia wajasiliamali wadogo na wakati
kuweza kuweka akiba zao kupitia simu zao za mkononi. Huduma hii pia
inawawezesha wateja wetu kukopa kupitia simu zao za mkononi ili kufungua fursa
mpya katika huduma za kifedha nchini.
Mwangalaba
alieleza “kupanuka kwa huduma za kifedha na kuwafikia wale watumiaji
wenye kipato cha chini ndio lengo halisi la Maendeleo benki. Mikakati yetu
tuliojiwekea ili kuwafikia wateja kama hao ni kuwapatia huduma nzuri na nafuu
zinazoendana na utoaji wa mikopo kwa makundi ili kuwapa uwezo wao wenyewe
waweze kudhaminiana kwenye makundi yao. Lengo letu Maendeleo Benki ni
kuhakikisha tunaendelea kuleta na kurahisisha zaidi huduma za kifedha kwa
kuweka mikakati kama hii itakayoleta tija katika maendeleo ya jamii nchini.
“Dhamira
yetu ni kuendeleza tabia ya kujiwekea akiba katika jamii na pia kuwapa wateja
uwezo wa kukopa na kupokea mkopo kupitia simu zao za mikoni kwa kuwa tunaamini
ni njia bora na rahisi zaidi kuliko ile iliyozoeleka. Mteja ukitumia huduma hii
ya mikopo ya Timiza Vikoba unajitengenezea historia
yako ya mkopo kidogo kidogo na baadae kujipatia mkopo mkubwa kwa masharti
rahisi zaidi “. Alimaliza kwa kusema Mwangalaba.
No comments:
Post a Comment