< span style="font-size: small;">Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Kongamano la kwanza la Biashara kati ya Ufaransa na Tanzania lililoandaliwa na Balozi wa Ufaransa nchini Bi. Malika BERAK (kulia), kushoto ni Mwenyekiti wa TPFS Dkt. Reginald Mengi.
< span style="font-size: small;"> Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akimsikiliza Balozi wa Ufaransa nchini Bi. Malika BERAK kabla ya kukaribishwa kuhutubia hotuba ya ufunguzi wa Wiki ya Kongamano la kwanza la
Biashara kati ya Ufaransa na Tanzania lililoandaliwa na Balozi wa
Ufaransa nchini linalo fanyika jijini Dar es Salaam.
< span style="font-size: small;">Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiangalia moja ya picha ya majengo yaliosanifiwa na wataalamu wa majengo kutoka nchini Ufaransa kwenye maonyesho ya Bisahara kati ya Ufaransa na Tanzania lililoandaliwa na Balozi wa
Ufaransa nchini
........................... .............................. .............................. .............
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesisitiza
kuwa Tanzania ni Moja ya nchi salama kwa ajili ya uwekezaji barani Afrika kwa
sababu haina matatizo ya migogoro ambayo yanaweza kuhatarisha usalama wa mali
ya wawekezaji ikilinganishwa na nchi nyingine barani Afrika.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli
hiyo wakati akifungua maonyesho ya Kibiashara kati ya Ufaransa na Tanzania
yanayofanyika Jijini Dar es Salaam.
Makamu
Rais Mhe Samia Suluhu Hassan pia amewakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji
kutoka nchini Ufaransa kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali hasa katika
kilimo, nishati, utalii,usafiri kutokana na hali ya amani na utulivu iliyopo
nchini.
Makamu wa
Rais amesema maonyesho hayo ya kibiashara ambayo yataambatana na kongamano
kubwa la Kibiashara kati ya nchi hizo Mbili ni fursa ya kipekee kwa
wafanyabishara wa Tanzania na Ufaransa kukutana na kubadilishana uzoefu katika
masuala mbalimbali ya kibiashara na uwekezaji.
Ameeleza
kuwa katika kuelekea katika uchumi wa viwanda Tanzania haiwezi kufanya kazi
hiyo peke yake bali kwa kushirikiana na mataifa makubwa ambayo yamekuwa na
teknolojia ya kisasa katika uwekezaji ikiwemo taifa la Ufaransa.
Makamu wa
Rais amewahakikishia wawekezaji wote wanaokuja kuwekeza nchini kuwa serikali
itafanya kila linalowekezekana kuendelea kujenga mazingira bora kwa ajili ya
uwekezaji.
Amesema
katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na mazingira bora ya uwekezaji barani
Afrika serikali imeendelea kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya kuimarisha
miundombinu mbalimbali ikiwemo bandari, reli, barabara, usafiri wa anga ili
kurahisisha kazi ya usafiri na usafirishaji nchini.
Kwa
upande wake, Balozi
Ufaransa hapa nchini Malika BERAK amesema kuwa ufunguzi wa Kongamano hilo kubwa
la Kibiashara kati ya Tanzania na Ufaransa linalolenga kujenga na Kuimarisha
ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo Mbili.
Balozi
huyo amesema kuwa kongamano hilo litajikita katika kujadili kwa kina fursa za
uwekezaji hapa nchini hasa kwenye maeneo ya nishati, usafirishaji, teknolojia
ya habari na Mawasiliano na miradi ya maendeleo.
Kongamano
hilo la siku Nne la Kibiashara kati ya Ufaransa na Tanzania
litawakutanisha wafanyabiashara wa Kitanzania na wenzao wa Ufaransa
katika kujadili na kubadilisha uzoefu katika masuala mbalimbali yakiwemo ya
kibiashara kama hatua ya kuimarisha shughuli zao za kiuchumi.
Imetolewa
na
Ofisi ya
Makamu wa Rais
;Ikulu-
Dar es Salaam.
4-April-2017.
No comments:
Post a Comment