Kaimu
Katibu Mkuu wa
Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka akizungumzia kadhia ya kuzuiwa kuswali waumini wa dini ya
kiislamu ambao ni wanachama cha chama cha mapinduzi ccm. (Picha Na Fahad Siraj)
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka akisikiliza taarifa ya kadhia ya kuzuiwa kuswali waumini wa dini ya kiislamu ambao ni wanachama cha chama cha mapinduzi ccm. (Picha Na Fahad Siraj)
Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka akisikiliza taarifa ya kadhia ya kuzuiwa kuswali waumini wa dini ya kiislamu ambao ni wanachama cha chama cha mapinduzi ccm. (Picha Na Fahad Siraj)
Wanachama wakimlaki Kaimu katibu mkuu mara baada ya kuwasili kuzungumza na wanachama wa Chama Cha
Mapinduzi na jumuiya zake katika mkutano wa ndani uliofanyika katika ukumbi wa
Jamhuri Wilayani Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Na
Mathias Canal, Kaskazini Pemba
Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM
umelaani vikali ubaguzi uliofanywa na baadhi ya Wanachama wasikuwa CCM kwa
kuwazuia wanachama wa CCM kuswali pomoja katika misikiti kwenye baadhi ya
maeneo Mbalimbali visiwani Pemba.
Umoja huo umesema kuwa kuzuia watu kuswali
kisa itikadi za dini zao ni dhambi kwa Mwenyezi Mungu kwani kufanya hivyo ni
kupiga amri ya Mwenyezi Mungu anayetoa onyo Kali katika Quran kwa wale
wanaothubutu kuwazuia waini wengine kuswali.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa
Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mpinduzi UVCCM Ndg Shaka Hamdu Shaka Wakati
akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi na Jumuiya zake Wakati
alipotembelea Msikiti wa Masjid Lmuhajiriina uliopo Eneo la Kiungoni Kimango
Wilayani Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Alisema kuwa Imani ya dini yoyote nchini
haibagui wala kuchagua watu kuswali kutokana na Itikadi zao za kisiasa ama
kikabila kwani dini Ni ibada ya Imani kwa kila mwananchi.
Shaka Alisema kuzuia watu kuabudu Ni makosa
kwa mujibu wa taratibu za nchi lakini pia ni Dhambi kwa Mwenyezi Mungu kwani
hakuna maandiko yanazuia watu kushiriki katika ibada.
Mnamo Mwaka Mwaka 2016 baada ya kura ya
marejeo kikundo Cha watu wachache katika baadhi ya maeneo walianza kuwashawishi
Wananchi kususia kuswali na Wanachama wanaotokana na CCM ambapo kwa kiasi
kikubwa waliwaunga mkono Jambo lililopelekea waumini was kiislamu watokanao na
CCM kuanza kusali majumbani mwao.
No comments:
Post a Comment