wadau wakionja ladha ya Whisky ya Johnnie Walker Black Label mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya kuitangaza mapema jana . |
Ni katika kuadhimisha miaka 20 ya Kampuni mama ya Diageo
Dar es Salaam
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza uzinduzi wa kampeni kwa ajili ya pombe kali aina ya Johnnie Walker (JW) Black Label inayojulikana kama, ‘JW Paints Tanzania Black’.
Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imetangaza uzinduzi wa kampeni kwa ajili ya pombe kali aina ya Johnnie Walker (JW) Black Label inayojulikana kama, ‘JW Paints Tanzania Black’.
Katika kampeni hii, shughuli
mbali mbali zitafanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kampuni
mama ya Diageo yatakayofanyika tarehe 15/12/2017. Diageo ndiyo mwana hisa
mkubwa kwenye kampuni ya SBL.
Ikiwa inatengenezwa na kampuni ya
Diageo na kusambazwa na SBL kwa hapa Tanzania, Johnnie Walker Black Label ambayo
ni Whisky ya Kiskoti inachukuliwa na wataalamu kama ndiyo whisky bora zaidi
duniani huku ikijali thamani ya pesa kwa watumiaji wake.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa
Masoko wa SBL Cesear Mloka, kampeni hiyo itaanza kwa programu ya kuongezewa
maarifa kwa wafanyakazi wa SBL ambayo itakwenda hadi katika ngazi ya marafiki,
wanafamilia pamoja na wadau wa biashara.
“Tunatarajia kuwa na tukio la
kufurahisha litakaloongozwa na wafanyakazi wetu ambao wataelezea ufahamu wao
pamoja na mapenzi yao kwa Johnnie Walker kwa watumiaji wa kinywaji hicho kwenye
sehemu mbali mbali kinapouzwa hapa nchini kama Bella Whispes, The Great, KB
Tabata,Green Palm,
Lachaz, MK, TIPS, Kuringe, Triple A, Front View, Dodoma Carnival na Golden
Crest.
Tukio hili halitafanyika hapa
Tanzania peke yake, bali linafanyika siku hiyo hiyo katika nchi 180 ambako Diageo
inafanya biashara zake na ambako Johnnie Walker Black Label inapatikana.
Tanzania ni sehemu ya kampeni ya kidunia
ya JW inayojulikana kama ‘Paint the World Black’ kuadhimisha shughuli hii yenye
mafanikio makubwa,” alisema Mloka wakati wa uzinduzi uliofanyika Dar es Salaam.
Mloka aliongeza kuwa, kampeni
hiyo itatangazwa kwenye magazeti, radio na televisheni, mitandao ya kijamii
pamoja na vyombo vya mawasiliano ya ndani ya kampuni.
Kampuni ya SBL pia imezindua maeneo
maalum ya kufanya manunuzi ya whisky ya Johnnie Walker Black Label mpaka
mwishoni mwa mwezi Disemba katika maduka ya vileo yaliyopo Dar es Salaam ya Kibong'oto,
Lamana, Master Liquor, Madeira & Herera pamoja na Arusha ya New Open Center
& Chware Stores. Johnnie Walker Black Label iliyoyachanganywa ina umri wa
miaka 12 na Ilitengenezwa wakati Johnnie Walker ikitimiza miaka 100 tangu
ilipotengenezwa kwa mara ya kwanza mwaka 1909. Ladha yake ni mchanganyiko wa
kipekee wa kimea, matunda, cocoa pamoja na vanilla.
Ikiwa inauzwa takribani kila nchi
duniani, ni whisky ya Kiskoti inayosambazwa zaidi duniani.
JW Black Label inakuja katika
kifungashio tofauti na endelevu (ikiwa kimstatili na nembo mbinjuko) huku
ikitoa fursa maridhawa nay a hali ya juu ya ufungashaji wa zawadi kwa wale
watumiaji wanaotazamia suluhisho la ufungashaji wa zawadi.
No comments:
Post a Comment