Tangazo

May 3, 2018

TANZIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi anasikitika kutangaza kifo cha Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Onesmo Mhewa kilichotokea jana jioni tarehe 02/05/2018.

Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili na unatarajiwa kusafirishwa kesho tarehe 04/05/2018 kwenda katika kijiji cha Nzihi kilichopo  Iringa vijijini kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika tarehe 05/05/2018.

Heshima za mwisho zitatolewa kesho tarehe 4/5/2018 katika ukumbi wa kufundishia uliopo chumba cha kuhifadhia maiti Muhimbili kuanzia saa 2 asubuhi hadi  saa 3  na baadaye nyumbani kwa kaka wa Marehemu kuanzia saa 6 mchana.

Kwa namna ya kipekee Prof. Janabi anatoa  pole kwa familia ya Marehemu, Wafanyakazi  wote, ndugu,  jamaa, marafiki  pamoja na wote walioguswa na msiba huu.

Msiba uko nyumbani kwa kaka wa marehemu Ndugu Lumumba Mhewa mtaa wa Mivumoni Madale.

“Bwana Ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe”.


Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete

03/05/2018

No comments: