Tangazo

August 9, 2011

Wabunge walivalia njuga suala la mgomo wa wauza mafuta

Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini January Makamba akitoa hoja yake binafsi ya dharura kuhusu tatizo la mafuta ya petroli nchini na ameitaka serikali kutoa tamko rasmi jinsi ya kumaliza tatizo hili ambapo wananchi wengi nchini wanapata taabu kuhusu usafiri katika maeneo mbalimbali.

Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela akichangia  Bungeni kuhusu tatizo la suala la mafuta kufuatia hoja ya dharura aliyoitoa Bungeni leo Mwenyekiti wa  Kamati ya Nishati na Madinim January Makamba kuhusu tatizo la mafuta nchini.


Baadhi ya wabunge wakiunga mkono  hoja ya dharura alioyoitoa Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini Januari Makamba kuhusu tatizi la mafuta nchini.

Mbunge wa  Kigoma Kaskazini Kabwe Zitto (Chadema) akichangia kuhusu sula la matatizo ya mafuta Bungeni leo ambapo ametaka serikali iwachukulie hatua wafanyabiashara watakaokuwa wakaidi kutii amri ya serikali kuhusu uzaji wa nishati ya mafuta.

Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja (kushoto) pamoja na Naibu wake, Adamu  Malima (kulia) wakiteta ndani ya ukumbi wa Bunge leo mjini Dodoma.

Waziri wa Viwanda na Biashara na Masoko,  Dk. Cyril Chami (kushoto) akiteta na Naibu Waziri wake, Lazaro Nyalandu kabla ya kusoma Bajeti ya Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko kuhusu Makadirio ya Mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2011/2012 leo Bungeni Dodoma. PICHA ZOTE/MWANAKOMBO JUMAA WA MAELEZO

No comments: