Tangazo

December 27, 2011

Serengeti Breweries Limited (SBL) yazindua Senator Extra Lager

Ni kitu kipya katika soko kinatambulishwa kwenu na kampuni ya Serengeti Breweries Limited ndani ya jiji la Mwanza, Kitu kinaitwa Senatar Extra Lager Bia ina alkohol 6 mwanawane.


Mkurugenzi wa masoko wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Ephraim Mafuru akizungumza katika uzinduzi wa bia mpya ya Senator Extra Lager ambayo imeanza kuzaliashwa na kusambazwa na kampuni hiyo. Bia hiyo inawalenga wachapakazi wa hali ya chini kabisa, wakulima, wavuvi na wengineo wa kanda ya ziwa na majirani zake. Bia ya Senetor itauzwa kwa bei nzuri ya shilingi elfu moja na mia tatu tu (1,300/-)

Watumishi wa SBL, mawakala na wadau wa kampuni hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo Ephraim Mafuru wakati wa uzinduzi wa bia ya Senator Extra Lager Jijini Mwanza.
                                           *********************************************
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua kinywaji kipya cha bia ya Senator, kinachozalishwa kwa kutokana na mazao ya mtama na shayiri na kuwataka wakulima wa mikoa ya Kanda ya Ziwa kulima mazao hayo kwa vile watakuwa na soko la uhakika.

Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika katika kiwanda cha SBL Mwanza hivi karibuni na kuhudhuruiwa na baadhi ya wafanyakazi,mawakala na wauzaji wa bidhaa za kampuni ya SBL. 
 
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uzinduzi wa kinywaji hicho kipya, Mkurugenzi wa Masoko wa (SBL) Ephraim Mafuru,alisema serikali inawaunga mkono kwa kusisitiza wakulima kuchangamkia kilimo cha mazao ya mtama na shayiri.

Alisema kuwa wakulima wa mikoa ya Kanda ya Ziwa wanapaswa kuanzisha kilimo cha mtama na kuuza mazao yao katika kiwanda cha SBL kinachozalisha kinywaji hicho na watakuwa na soko la uhakika.

“Tunaagiza malighafi kutoka nje ya nchi kwa asilimia 80 ili kukidhi mahitaji kwa sababu asilimia 20 ya malighafi ya hapa nchini ni ndogo,hivyo wakulima wa Kanda ya Ziwa wanapaswa kulima na kuuza mazao yao kiwandani kwetu na wao kunywa kinywaji hiki cha Semator ili kusukuma biashara hii.Soko la mazao yao kama mtamama na mahindi linapatikana SBL ambapo tumekuwa tukinunua kilo moja ya mtama kwa shilingi 600,”alisema Mafuru.

Alisema kuwa bia ya Senator yenye kilevi cha asilimia 6 inazalishwa kutokana na kimea cheupe kinachotokana na mtama, kinywaji ambacho kimemlenga mtanzania wa kipato cha kawaida wa mikoa ya Kanda ya Ziwa. 
 
Alieleza kuwa kinywaji hicho tayari kipo sokoni na kuwataka wateja wake ambao ni wavuvi na wakulima kukinunua ambapo bei ya mlaji itakuwa ni shilingi 1300,ambapo Januari mwakani watafanya matamasha ya kukitangaza kinywaji hicho zaidi katika maeneo ya vijijini.

Aidha alisema kauli mbiu ya kinywaji hicho ni ‘bia ya wachapakazi ahsante kwa kutuwezesha kuwa kampuni kubwa’ ambapo SBL inatarajia kudhamini ngoma za utamaduni za makabila ya Wasukuma za Wagika na Wagalu. 
 
Kwa upande wake Meneja Mauzo wa SBL Kanda ya Ziwa, Stansaus Theophile, alisema bei tishari moja ilenye chupa 25 liytauzwa kwa bei ya shilingi 25 kwa mawakala,shilingi 25,400 (mawakala wa kati) na shilingi 26,000 kwa mawakala wadogo na mlaji shilingi 1300.

No comments: