Tangazo

December 12, 2011

Wasanii Nyota wazindua Airtel Money mjini Dodoma

Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Sir Juma Nature (katikati) akishiriki uzinduzi wa Airtel Money ndani ya mji wa Dodoma jioni ya leo kwenye uwanja wa Jamhuri, ambapo watu mbalimbali walijitokeza kwa wingi kulishuhudia tukio hilo adimu. Kulia ni Meneja Mawasiliano wa kampuni ya Airtel, Jackson Mmbando na (kushoto) ni Meneja wa Airtel Money-Tanzania, Asupya Bussi Nalingingwa.

Msanii mahiri wa miondoko ya hip hop, Hamis Mwinjuma a.k.a Mwana FA akiwapagawisha baadhi ya wakazi wa mji wa Dodoma waliofika jioni ya leo kwenye tamasha la uzinduzi wa huduma ya Airtel Money, uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma na kuhudhuriwa na watu kibao.

Namna shangwe za Aitel Money zilivyokuwa zikilindima usiku huu ndani ya Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

'Simba Dume' ndani ya msitu mnene ni mmoja ya Wasanii wakongwe wa hip hop hapa nchini, ndani ya miondoko ya muziki wa kizazi kipya, Mfalme wa rhymes Afande Seleman Msindi 'Afande Sele' (mwenye rasta) akiwa amezungukwa na washabiki wake huku akiwaimbia wimbo wake wa Karata Dume, shangwe na miluzi ikiwa imetawala uwanjani hapo jioni ya leo,wakati kampuni ya simu ya mikononi ya Airtel ilipokuwa ikizindua huduma yake mpya ya Airtel Money kwa wakazi wa mji wa Dodoma jioni ya leo. 

No comments: