Tangazo

December 12, 2011

KLABU ZA JOGGING ZA KINONDONI ZASHEREHEKEA MIAKA 50 YA UHURU KWA KUFANYA USAFI MWANANYAMALA HOSPITALI



Wanachama wa Klabu za Jogging za Wilaya ya Kinondoni wakiwa katika mbio maalum kwa ajili ya kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru, zilizoanzia katika Viwanja vya Biafra hadi Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam jana ambapo walishiriki kufanya usafi hospitalini hapo na kutoa misaada ya vyakula na vitu mbalimbali. Vilabu vilivyoshiriki ni Biafra Sports Club, Namanga sports Club na Kunduchi Kwanza Sports Club.PICHA ZOTE/JOHN BADI


Wanachama wa Klabu za Jogging za Wilaya ya Kinondoni wakifanya usafi katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam jana ikiwa katika kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru, baada ya kukimbia mbio maalum zilizoanzia katika Viwanja vya Biafra hadi hospitalini hapo na kutoa misaada ya vyakula na vitu mbalimbali. Vilabu vilivyoshiriki ni Biafra Sports Club, Namanga Sports Club na Kunduchi Kwanza Sports Club.


Wanachama wa Klabu za Jogging za Wilaya ya Kinondoni wakitoa misaada ya vyakula na vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam jana ikiwa katika kusheherekea Maadhimisho Miaka 50 ya Uhuru, baada ya kukimbia mbio maalum zilizoanzia katika Viwanja vya Biafra hadi hospitalini hapo na kutoa misaada ya vyakula na vitu mbalimbali. Vilabu vilivyoshiriki ni Biafra Sports Club, Namanga sports Club na Kunduchi Kwanza Sports Club. Pichani ni Mwenyekiti wa Kunduchi Kwanza Sports Club, Asia Mohamed

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Abdu Mollel (wa pili kulia) akikabidhi sehemu ya msaada wa vyakula na vitu mbalimbali kwa Ofisa Muuguzi wa Zamu wa Hospitali ya Mwananyamala, Angela Magesa wakati Wanachama wa Klabu za Jogging za Wilaya ya Kinondoni walipokwenda Hospitalini hapo jijini Dar es Salaam jana kufanya usafi baada ya kukimbia mbio maalum zilizoanzia katika Viwanja vya Biafra ikiwa katika kusherehekea Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru,. Vilabu vilivyoshiriki ni Biafra Sports Club, Namanga sports Club na Kunduchi Kwanza Sports Club. Katikati ni Mkurugenzi wa Klabu ya Biafra, Asha Mweke na (kulia), ni Mwanachama wa Klabu ya Namanga, Mzee Siara.

No comments: